Na Imma Msumba ; Arusha
Akizungumza katika ziara hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo Ezra Chiwaleza ambaye ni Mbunge wa Biharamulo amesema wanampongeza sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya na kutoa pesa nyingi anazoendelea kuwapatia katika wizara ya kilimo “kama tulivyoona mradi huu wa ASA uliopo Ngaramtoni kazi inayoendelea ni kubwa bwawa limechimbwa na liko katika hali nzuri na kufikia katika hatua ya umaliaziaji .
“Pia tumpongeze mkandarasi anayefanya kazi hii kazi inaridhisha kama kamati tumefika hapa tumeona kazi ni nzuri na tunampongeza pia mkurugenzi kwa kazi kubwa anayoifanya “alisema
Kikubwa sisi tumewahasa kwa yale ambayo wanaona kwamba wanayaitaji kama kamati ilikuweza kuifikia ndoto ya Rais kwenye kuwahudumia watanzania wayalete kazi ya kamati tunapokuja hapa hatuji kama mahakimu tunakuja kuona changamoto ambazo wanazo watendaji hususani taasisi ambazo ziko chini ya wizara ili twende tukaseme kwa niaba yao kama kamati inayosimamia wizara hizi ili pesa inayoitajika iweze kupatikana kwaajili ya kufanya utekelezaji.
Kamati imeridhika na miradi inayoendelea hapa miradi ni mizuri tunazidi kuwauunga mkono kwahiyo wafanye haraka kwa wale ambao wanayo ili kamati hii chini ya mwenyekiti wetu tuone ni jinsi gani tukashauri serikali ili yale ambayo yanaitajika kwaajili yakuweza kuongezea nguvu yaongezewe nguvu ili waweze kuwahudumia watanzania maana kazi inayofanywa na ASA ni kuhakikisha watanzania wanapata mbegu bora ilipale unapolima eneo dogo uweze kuzalisha kwa wingi.
“Sasa kama kazi hii haitafanyika maana yake watanzania wataumia watakuwa wanatumia mbegu zilezile za kienyeji unalima hekari ishirini unavuna kidogo ila aliyelima hekari tano anavuna zaidi yako wewe”aliongezea
Naye Naibu waziri wa kilimo Ernest Silinde ameeleza kuwa wizara inafanya kazi kwa karibu na kamati hiyo na inajukumu la kupitisha fedha na moja ya jukumu lao ni kuangalia maendeleo ya mradi na kushauri kwa kutoa mapendekezo kulingana na kile walichokiona.
“Niwahakikishie kamati ya bunge kwamba maoni yao ushauri wao wote walioutoa sisi kama wizara tumeyapokea na tutakwenda kuyafanyia kazi kama ambavyo tumekuwa tukifanya hivyo mara kwa mara”
Hata hivyo nipende kuwaeleza watanzania mashamba haya ni kazi nzuri inayofanywa na Dkt. Samia hayani maono yake ni maoni ya Ilani ya chama cha mapinduzi maono haya yanayofanyika hapa yamekusudia jambo moja kuongeza uzalishaji wa mbegu bora hapa nchini kwasababu tunahitaji mbegu bora na zauhakika katika muda wote wa msimu.
"Tumekuwa na changamoto ya mbegu kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia fedha za kigeni kuagiza mbegu nchini kwahiyo tukiongeza uzalishaji maana yake tutapunguza matumizi ya fedha za kigeni nje ya nchi mpaka kufikia 2030 tuwe tumeondoa uhaba wa mbegu nchini." Aliongezea
Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella,ameiomba kamati hiyo kuhakikisha mashamba 11 yawawekezaji yaliyorudishwa serikalini takribani miaka mitano iliyopita wayafanyie mpango iliyaweze kurudi katika wizara ya kilimo ili yakaendelezwe kwani soko la dunia ya sasa linataka mbogamboga na maua “mwenyekiti wa kamati shamba moja lilikuwa linaajiri zaidi ya wafanyakazi elfu moja asilimia 90 ya wafanyakazi hao walikuwa ni wanawake na vijana ”alisema