SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO - RC MNDEME

 


Na Shinyanga RS.

MKUU wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amefanya kikao kazi na Maafisa Tarafa, watendaji kata, mitaa na vijiji kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kazi ikiwemo kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, utatuzi wa kero za wananchi, kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato, kueleza umma juu ya fedha wanazopokea kutoka serikali kuu, utunzaji wa mazingira na kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 10 Oktoba, 2023 wakati alipokutana na wataalam hao katika ukumbi wa mikutano uliopo shule ya savannah plains huku akiwasisitiza kwenda kuzingatia maadili na nidhamu huku akikemea tabia ya kuchati na simu wanapokuwa wakiwahudumia wananchi huku akisisitiza kuwa kipaumbele cha serikali ni utoaji wa huduma bora kwa wananchi wenyewe na ndiyo maelekezo ya Mhe. Rais.

"Nendeni mkasimamie utekelezaji wa miradi ya maendeleo, mkatoe elimu juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira, tatueni kero za wananchi, toeni taarifa za mapokezi ya fedha za serikali pia mkaongeze bidii katika kukusanya wamapato ya serikali katika maeneo yenu," alisema Mhe. Mndeme.

Katika hatua nyingine Mhe. Mndeme amewaeleza wataalam hao kuwa serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta zaidi ya Trilioni moja fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali huku akiwataka kwenda kuzisimamia ili zililete matokeo chanya kwa wananchi katika maeneo yao.

Aidha amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huu kuhakikisha wanalipa stahiki za watumishi wao, kuandaa mafunzo ya watumishi, kutatua kero za wananchi na watumishi katika halmashauri zao ili wamsaidie Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndiyo maelekezo yake huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidiii zaidi.

Kwa upande wao wakurugenzi wa halmashauri hizi za mkoa wa shinyanga wamekiri kupokea maelekezo ya Mhe. Mndeme na kumuahidi kuwa wanakwenda kuyatekeleza maelekezo yote ikiwemo utatuzi wa migogoro na kulipa stahiki za watumishi wao.

@ortamisemi @christinamndeme18 @shinyangamanispaa @kishapudc @shinyangadc_

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post