Mshindi wa kwanza katika Shindano la Shindano la Stories of Change,Athanas Myonga akikabidhiwa mfano wa hundi aliyoshinda
Mshindi wa kwanza katika Shindano la Shindano la Stories of Change,Athanas Myonga akizungumza katika Usiku wa Tuzo za Shindano la Uandishi wa Mtandaoni.
Mshindi wa pili Respick Tairo Hugolini, na Nathanie mshindi wa tatu na wa nne ni BASHARI N. KIDAYA na Nick Rusule wa akikabidhiwa mfano wa hundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akizungumza katika Shindano la Shindano la Stories of Change.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza na Charlotta Ozaki ambaye ni Balozi wa Sweden.
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo (kushoto) akiwa na Msanii Banana Zorro wakati wa Utoaji Tuzo za Shindano la Stories of Change kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2023.
Charlotta Ozaki (Balozi wa Sweden) wakati akitoa hotuba kwenye utoaj wa Tuzo za Shindano la Stories of Change.
*******
Na Mwandishi Wetu
Athanas Myonga amefanikiwa kuwa Mshindi wa kwanza katika Shindano lililoandaliwa na Taasisi ya Jamii Forums ambapo Wananchi mbalimbali walipata nafasi ya kuandika maandiko yenye lengo la kusaidia jamiii katika Utawala Bora na Uwajibikaji.
Mshindi huyo amepata ushindi wa andilo lililolenga kutoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu kupanga Malengo ya Fedha zinazokusanywa, ambapo amejizolea kitita cha fedha taslimu Tsh. 7,000,000/-
Akizungumza katika Usiku wa Tuzo za Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change) Msimu wa Tatu (Stories of Change 2023, Myonga amesema ameweza kuandika andiko LA Namna ya kupanga malengo ya fedha za kukusanya ili TRA kuwe na uwajibikaji,.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mobhare Matinyi amesema Serikali ya Awamu ya 6 inatambua umuhimu wa kushirikisha Wananchi katika kuimarisha Utawala Bora na upatiakanajinmwa taarifa Nchini.
Maxence Melo ni Mkurugenzi Mtendaji JamiiForums amesema hatua Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka 5 ya kuinua sauti za Wananchi na kuimarisha Upatikanaji wa Taarifa kama moja ya maeneo yetu muhimu ya kimkakati.
Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Balozi wa Sweden, Charlotta Ozaki, pia Mabalozi wengine walihudhuria ni Balozi wa Marekani, Dkt. Michael Battle Sr, Balozi wa Denmark - Mette Norgaard.
Wengine waliokabidhiwa zawadi katika Usiku wa Tuzo uliofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es a Salaam ni mshindi wa pili ni Respick Tairo Hugolini aliyepata Tsh. 4,000,000, Nathaniel amekuwa mshindi wa tatu akijizoea Tsh. 3,000,000, wa nne ni BASHARI N. KIDAYA aliyepata Tsh. 2,000,000 na wa tano ni Nick Rusule aliyepata Tsh. 1,000,000