Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AJALI YA BASI LA ALFA, LORI YASABABISHA VIFO VYA WATU 18 NZEGA

 

Watu 18 wamefariki dunia na wengine 35 kujeruhiwa baada ya basi la Alfa walilokuwa wakisafiria kugongana na lori la mafuta mjini Nzega mkoani Tabora.


Akitoa taarifa ya ajali hiyo leo Jumamosi Oktoba 21, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la Alfa linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam na kwamba wakati wa ajali, lilikuwa likitokea Shinyanga.

"Nimepata taarifa hiyo na sasa ndio naelekea eneo la tukio na taarifa kamili nitaitoa baada ya kufika na kujua hali ilivyo," amesema

Chanzo Mwananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com