Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC GAILO AWATAKA WAFUGAJI KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA CHANJO ZA MIFUGO

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Masoko na Habari kutoka Wakala Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bw. Prosper Haule akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA kujifunza kazi zinazofanywa na TVLA pamoja matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo zinazozalishwa na TVLA kwenye maonesho ya pili ya Kilimo Biashara na Kilimo Marathon 2023 yanayofanyika Gairo Kata ya Chakwale Mnadani Mkoa wa Morogoro Oktoba 13, 2023. Kulia kwake ni Mtaalamu wa TVLA kituo cha Dodoma Bw. Anastasius Ngatata
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Kanda ya Kati Dodoma Dkt. Japhet Nkangaga (mwenye miwani) akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA kujifunza kazi zinazofanywa na TVLA pamoja matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo zinazozalishwa na TVLA kwenye maonesho ya pili ya Kilimo ni Biashara Kilimo Marathon 2023 yanayofanyika Gairo Kata ya Chakwale Mnadani Mkoa wa Morogoro Oktoba 13, 2023. Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Masoko na Habari wa TVLA Bw. Prosper Haule.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Y. Nabalangana (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Wakala kwenye maonesho ya pili ya Kilimo Biashara na Kilimo Marathon 2023 yanayofanyika Gairo Kata ya Chakwale Mnadani Mkoa wa Morogoro Oktoba 13, 2023. Waliosimama kutoka kulia ni Meneja wa TVLA Kanda ya Kati Dodoma Dkt. Japhet Nkangaga na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Masoko na Habari wa TVLA Bw. Prosper Haule.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri O. Makame (kulia) akipata maelezo kuhusiana na matumizi sahihi ya aina 7 za Chanjo zinazozalishwa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kutoka kwa Meneja wa TVLA Kanda ya Kati Dodoma Dkt. Japhet Nkangaga alipotembelea banda la TVLA kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Wakala kwenye maonesho ya pili ya Kilimo Biashara na Kilimo Marathon 2023 yanayofanyika Gairo Kata ya Chakwale Mnadani Mkoa wa Morogoro Oktoba 13, 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com