DC TANGA AZINDUA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO AIPONGEZA TAASISI YA ANSAAR MUSLIM KWA KUJITOA KWA JAMII




Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyani  wakati alipokwenda kuzindua zoezi la uchangiaji damu salama lililoratibiwa na Taasisi hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Athumani Kihara,ambapo vijana wa taasisi hiyo 600 wanatarajiwa kushiriki kwenye zoezi hilo kulia ni Mwenyekiti wa Idara ya Ustawi wa Jamii katika Taasisi ya Ansaar


MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo na kulia ni Matroni wa Hospitali hiyo Beatrice Rimoy

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Athumani Kihara akizungumza wakati wa halfa hiyo



Zoezi la Uchangiaji damu likiendelea


Zoezi la Uchangiaji damu likiendelea

Sehemu ya vijana kutoka Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji ambaye hayupo pichani


MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu mapema leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo
MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu mapema leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo

MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji katikati akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyan mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Taasisi hiyo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Athumani Kihara


Na Oscar Assenga, TANGA.

Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji leo amezindua zoezi la uchangiaji watu wanaochangia damu kwa wahitaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

Zoezi hilo lililokuwa limeratibiwa na Taasisi ya Ansaar Muslm Youth Centre kupitia Idara yake ya Ustawi wa Jamii Makao Makuu amba wameshirikiana na kituo cha Mahad Imam Shafii Tanga ambapo zaidi ya vijana 600 wanatarajiwa kuchangia damu.

Akizungumza mara baada ya kulizindua zoezi hilo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kitengo cha taasisi hiyo kutoa damu wamefanya jambo kubwa la dhawabu kuliko kitu chochote.

Alisema kwamba kwani wanapofanya hivyo wanawezesha kuwasaidia watu wengine wenye uhitaji ambao wanakumbana na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowahitaji kuongezewa damu.

“Niwapongeze sana na niwaambie kwamba jambo mnalolofanya hapa ni kubwa mnoo kutokana na kwamba unasaidia jamii yenye uhitaji”Alisema

Aidha alisema kwamba ni watu wachache ambao wanaweza kubuni jambo hilo hivyo niendelea kuiasa jamii kuwa na mwamko wa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuwa sehemu ya kusaidia wenye uhitaji.

“Niwapongeze kwa kuona umuhimu wa kuchangia damu nyie mmekuwa kuokoa maisha ya watu wengine kwani wakati mwengine wanapoteza maisha wengine hata ndugu zao wanaogopa kuwatolea damu lakini nyie mmejitoa hii ni sadaka kubwa asanteni sana”Alisema

Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba waandishi wa habari kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa jamii.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyan alisema taasisi hiyo kwa niaba ya vijana wao wameamua kujitokea damu kwa ajili ya wagonjwa.

Alisema huo ni utaratibu wao ambao wamekuwa wakiufanya mara kwa mara kusaidia jamii yenye uhitaji kwa kuhakikisha wanachangia damu katika maeneo mbalimbali.

Aidha alisema uanzishwaji wa taasisi hiyo malego yake ni kuelimisha jamii, kuhudumia jamii pamoja na kwamba ni taasisi ya kidini lakini wanatoa mafunzo hazimu ya mtume wao.

Alisema katika mafunzo hayo sio kwamba dini ni ibada tu bali ni huduma kwa jamii na yamekuja mafunzo mengi sana kuhusu umuhimu wa kuwasaidia wanyonge wa aina zote,masikini,walemavu.

“Lakini pia tunasaidia watu wenye mahitaji maalumu, waliopata matatizo ya kiafya wa aina zote za unyonge na sisi ndio mafunzo tunayopewa na mtume kuhudumia jamii na katika jumla ya kuhudumia jamii ni kuchunga afya za watu kwa sababu ibada haziwezi kufanyika kama watu ni wagonjwa”Alisema

Hata hivyo alisema pampoja na kwamba wao wamebobea katika masuala ya kielimu lakini huduma za jamii upande wa afya wameziona ni muhimu sana na walishawahi kufanya kambi mbalilmbali za kuwahudumia watu hasa wa macho kwa kutumia wataalamu wa ndani.

Pia alisema wao wamekuwa mstari wa mbele kuifikia jamii kwenye zoezi la kujitokea damu na litakuwa ni endelevu kwenye mkoa wa Tanga na nje ya mkoa huo.


Naye kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Athumani Kihara aliwashukuru Taasisi ya ya Ansaar Muslim Youth Centre kwa jambo ambalo wamelifanya kwa kujitolea huduma ya damu kwa wahitaji.

Dkt Kihara ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wakina mama na Uzazi alisema kwamba jambo wanalo lifanya ni muhimu sana kwa jamii kutokana na kwamba katika idara ambazo zinaathirika sana suala la damu ni la uzazi.

Alisema wamekuwa wakipata matatizo mengine ya wakina mama wamekuwa wakipata kutokana na upungufu wa damu kipindi cha ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua matatizo mengi yakiwemo moyo na figo .

Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Maabara Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Sinde Mtobu alisema mwaka huu hamasa imeendelea kuwa kubwa kwa mwezi sasa wastani wanapata chupa 600 kwa mwezi.

Alisema hali hiyo imepunguza gepu la wahitaji ingawa bado wapo wahitaji wapo hivyo niwapongeze sana na wanawaomba waendelee kuwa pamoja nasi.


Hata hivyo alisema ikiwa kwenye Taasisi kila jamii yenye watu ikiwa na tukio la kuchangia damu mara moja tu kwa mwaka hakika changamoto ya damu itakuwa imekwisha hivyo wataendelea kushirikiana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post