Na Mwandishi Maalum,Dar Es Salaam
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko anatarajia kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini mwaka 2023, leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo unahudhuriwa na Viongozi, Washiriki na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi na unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkutano huo, unatarajiwa kutangaza fursa mbalimbali ya Madini Mkakati na Madini muhimu yaliyopo hapa nchini.
Social Plugin