Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAPANI YAIPIGA JEKI SHULE YA MSINGI KIBOHEHE KILIMANJARO



Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa, kulia akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri wakikata utepe kwenye madarasa 8 na ofisi mbili zilizotolewa na ubalozi huo.



Mkuu wa shule ya Kibohehe Flora Nathaia, akimkabidhi zawadi ya mchoro wa shule hiyo Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa.


Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa akisalimia na viongozi wa Wilaya ya Hai ya mkoani Kilimanjaro wakati wa makabidhiano ya madarasa 8 na ofisi mbili za walimu katika Shule ya Msingi Kibohehe.



Wanafunzi wa shule ya Msingi Kibohehe wakisoma ushahili mbele ya Viongozi wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na Balozi wa Japani Nchini Tanzani Yasushi Misawa.


Miongoni mwa madawati katika shule ya Msingi Kibohehe ambayo pia ni udhamini wa ubalozi wa Japani Tanzania.
(PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY)
********


Ubalozi wa Japani Tanzania umekabidhi vyumba vya madarasa 8 na ofisi mbili za walimu Vyenye thamani ya shilingi milioni 204 Kwa shule ya Msingi Kibohehe iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.


Akikabidhi madarasa hayo shuleni hapo Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa amesema kuwa wametimiza ahadi ya Ujenzi wa Madarasa hayo na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri na salama ya kusoma na kujifunza.


Vyumba hivyo vimejengwa na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania kufuatia kuanguka kwa darasa na kusababisha kifo Cha Mwanafunzi Mmoja mwaka 2018.

"Leo, nina furaha kuona jengo jipya la madarasa limekamilika kwa mafanikio na zaidi ya wanafunzi 200 wanafurahia kusoma hapo." Alisema balozi Misawa


Balozi Misawa amewasihi walimu na wanafunzi wa shule hiyo kutumia ipasavyo na kudumisha ipasavyo madarasa hayo kwa muda mrefu ili kuchangia maendeleo zaidi ya watoto wa kijiji hicho.


Aidha amesema Serikali ya Japan imekuwa ikitoa misaada ya mara kwa mara katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania na kudai kuwa kukabidhi madarasa hayo ni hatua nyingine katika kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan.


Awali Mkuuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa akimkaribisha balozi aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo wa Ujenzi wa shule nzima na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.


"Mheshimiwa Balozi tunakushukuru wewe na Serikali ya Japan kwa msaada huu muhimu wa Ujenzi wa shule nzima ya Kibohehe mara baada ya madhila yale tuliyopata mwaka 2018, madarasa haya yatakuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya Elimu" Alisema Mkalipa.


Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Kibohehe, Flora Nathai amesema ilikuwa ni huzuni kubwa tarehe 21 February, 2018 baada ya mvua kubwa kunyesha na kuezua paa na kuangusha ukuta wa darasa uliosababisha kifo Cha Mwanafunzi Mmoja Derick Albert na kujeruhi wanafunzi wengine watano na kuleta simanzi kubwa kijijini hapo, Hali iliyopelekea kufungwa Kwa shule hiyo na kuwahamishia wanafunzi wote katika shule za jirani.


Amesema shule hiyo ina wanafunzi 224 ambapo wavulana ni 109 na wasichana 115 Ina walimu 9 kati yao mwalimu wa kiume ni Mmoja na nane ni wanawake.


Balozi wa Japan kafanya ziara ya kukagua Miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Japan pamoja na shirika la kimataifa la msaada la Japan (JICA) katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.


=MWISHO=




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com