Meneja wa Programu wa LSF Bw.Deogratius Bwire akipokea Cheti cha pongezi kutoka kwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango kama Shirika bora linalosaidia ukuaji wa Mashirika madogo yasiyo ya kiserikali nchini katika hafla ya ufungaji wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali mkoani Dodoma.
***************************
Shirika la Legal Services Facility (LSF) linalojishughulisha na uwezeshwaji wa upatikanaji wa haki nchini limetunukiwa cheti cha pongezi kwa kuwa shirika linalofanya vizuri katika kujengea uwezo mashirika madogo nchini. Cheti hicho kimekabithiw na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango katika Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali la mwaka 2023 lililofanyika jijini Dodoma
Kutunukiwa kwa cheti hicho kumetokana na juhudi zinazofanywa na LSF kwa takribani miaka 12 sasa katika kutoa ruzuku kwa mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 200 Tanzania bara na Zanzibar na pia kuyajengea uwezo wa kuwa na mifumo, kuwapatia ueledi kwenye maswala ya kifedha, kiprogram, utendaji, uongozi, kuonyesha matokeo. Aidha LSF imekuwa ikitoa elimu ya mara kwa mara kwa mashirika hayo hususani ya msaada wa kisheria juu ya sheria na mabadiliko yake ili kazi kwa ueledi katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchini hussani wanawake na watoto
Mafanikio ya LSF yamewezeshwa chini ya ufadhil wa wadau wa maendeleo Ubalozi wa Dernmark na pia Umoja wa Ulaya. Ufadhili ambao umeleta tija kuja katika kuwezesha upatikanaji haki kupitia huduma za msaada wa kisheria bila gharama yoyote katika kila mkoa na wilaya ya Tanzania bara na Zanzibar
Akiongea kuhusu tuzo hiyo Mkurugenzi Mkuu wa LSF bi Lulu Ng’wanakilala amesema wamepokea kwa heshima kubwa pongezi hizo kutoka kwa Serikali chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Wazee, watoto na makundi maalumua nakushukuru kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na LSF katika kuchochea haki kwa wote lakini pia katika kuyajengea uwezo na kuyapatia ruzuku mashirika yasiyo ya kiserikali nchini na kuongeza kwamba watandelea kushirikiana na Serikali, wadau wa maendeleo ,mashirika binafsi pamoja na wadau wengine wengi ndani na nje ya nchi katika kutatua changamoto za wananchi hususani wanawake na watoto wakike ambao ndio waanga wakubwa wa vitendo vya ukosefu wa haki
“Tumepokea kwa furaha cheti hiki na tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wetu kwa kuwajengea uwezo na kuwawezesha kuwafikia wananchi wengi hususani walio maeneo ya pembezoni mwa nchi. Sambamba na hili sisi kama wadau wakubwa katika sekta hii tutaendelea kushirikiana na Baraza la Taifa la Mashirika Nchini NACONGO pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii katika kuandaa mkutano huu wa mwaka ili kuyanapata jukwaa mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini pamoja na Serikali kuzungumza maswala muhimi ikiwemo mafanikio, changamoto na fulsa zilizopo katika undeshaji na utoaji huduma kwa wananchi. niwapongeze sana NACONGO pamoja na ofisi ya Msajili wa NGO nchini kwa kazi kubwa na nzuri ya kutuleta pamoja ila mwaka” alisema Ng’wanakilala
Jukwaa la mashirika yasiyo ya kisherikali lilifungwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango aligusia mambo mengi ikiwemo; kusisitiza kwa mashirika yasiyo ya kiserikali Kuzingatia uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji miradi,Kuzingatia maadili ya kitanzania kwa kuheshimu mila na desturi za Tanzania na pia kufuata sheria na miongozo iliyowekwa nakuagiza baada ya mkutano utengenezwe mpango mkakati ambao changamoto zote zitaainishwa na mamlaka za utekelezaji.
Social Plugin