Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAUZO YA HATIFUNGANI YA KIJANI YA BENKI YA CRDB YAVUKA MALENGO, CMSA YATOA PONGEZI


Na Mwandishi Wetu

OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) CPA.Nicodemus amesema mauzo ya toleo la kwanza la kijani ya Benki ya CRDB yaliyofunguliwa Agosti 31,2023 na kufungwa Oktoba 6,2023 yawewezesha kupatikana kwa Sh.bilioni 171.83 ikilinganisha na kiasi Sh.bilioni 40 zilizotarajiwa kupatikana.

Sawa na mafanikio ya asilimia 429.57 kufukia Sh.bilioni 177.83 huku CMSA ikiidhinisha benki ya CRDB kutumia kiasi chote kilichopatikana kutokana na uwepo wa mahitaji ya kutosha kugharamia miradi inayokidhi matakwa ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Akizungumza leo Oktoba 27,2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuorodheshwa kwa toleo la kwanza la hatifungani ya Benki ya CRDB katika Soko la Hisa Dar es Salaam CPA.Mkama amesema kama inavyofahamika Serikali imaweka mkakati wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa wote ambao ni rafiki kwa mazingira , hivyo utoaji wa hatifungani hiyo ya CRDB unawezesha utekelezaji wa malengo na azma ya serikali katika nishati safi.

“Kadri taifa letu linavyosonga mbele katika utekelezaji wa mpango wa tatu wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/2026 wenye dhima ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu mahitaji ya rasilimali fedha ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii na uchumi hususa miradi ya miundombinu inayotunza mazingira inaongezeka,”amesema.

Ameongeza ili kufanikisha azma hiyo ifikiwe kunahitajika uwepo wa bidhaa mpya bunifu ambazo zinaleta anuai katika masoko ya fedha ikiwa ni pamoja na hatifungani za kampuni kama hatifungani ya kijani iliyotolewa na benki ya CRDB.

Aidha amesema mauzo ya hatifungani hiyo yamekuwa na matokeo chanya katika maendeleo ya sekta ya fedha hapa nchini ambapo asilimia 98 ya wawekezaji walioshiriki ni wawekezaji mmoja mmoja na asilimia mbili ya wawekezaji ni kampuni na taasisi

Pia asilimia 99 ya wawekezaj ni wawekezaji wa ndani na asilimia moja ni wawekezaji wa nje wakati kwa upande wa kiasi kilichopatikana asilimia 51 inatoka kwa wawekezaji mmoja mmoja na asilimia 49 inatoka kwa kampuni na taasisi.

“Asilimia 62 ya kiasi kilichopatikana inatoka kwa ushiriki wa wawekezaji mmoja mmoja wa ndani na asilimia 38 inatoka kwa wawekezaji wan je ya nchi.Ushiriki wa wawekezaji mmoja mmoja wa ndani ni hatua muhimu katika kuongeza ukwasi katika soko…

“Na utekelezaji wa mpango jumuishi wa huduma za kifedha wenye lengo la kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye sekta rasmi ya fedha.Hivyo tunakila sababu ya kuipongeza CRDB na wadau wote walioshiriki katika kuwezesha mafanikio haya.

“Mauzo ya hatifungani hii ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mpango mkuu wa maendeleo wa sekta ya fedha wenye lengo kwa asilimia 20.29 na kufikia Sh.trilioni 19.71 katika kipindi kinachoishia septemba 2023 ikilinganishwa na Sh.trilioni 16.30 katika kipindi kinachoishia septemba 2022.”

CPA.Mkama amesema kwa mantiki hiyo leo hatifungani ya CRDB imeorodheshwa sokoni huku akifafanua thamani ya uwekezaji katika hatifungani za kampuni inaongezeka kutoka Sh.bilioni 153.56 na kufikia Sh.bilioni 325.39 sawa na ongezeko la asilimia 111.89

Hivyo amesema wana kila sababu ya kuipongeza benki ya CRDB na taasisi ya watalaam wote walioshriki katika kuwezesha mafanikio haya.

“Pamoja na mambo mengine uorodheshwaji wa hatifungani hii katika soko la hisa unawapatiwa fursa wawekezaji kuuza hatifungani zao pale wanapohitaji fedha kwa ajili ya matumizi mengine, kujua thamani halisi ya hatifungani zao na kuwapatia fursa wawekezaji wapya kununua hatifungani hizo ambapo wawekezaji hao hupata riba kama faida itokanayo na uwekezaji huo,”amesema.

Aidha uorodheshwaji wa hatifungani za kampuni unaongeza utawala bora na ufanisi katika uendeshaji wa kampuni na kumwongeza mwekezaji wigo na fursa za uwekezaji .Hiyo inamsaidia mwekezaji kuwa na anuwai jambo ambalo hupunguza athari za uwekezaji .

Ameongeza pia uwepo wa bidhaa nyingi ,mpya na bunifu katika masoko ya mitaji unachangia utekelezaji wa mkakati wa serikali wa njia mbadala za kugharamia miradi ya maendeleo wenye lengo la kuwezesha Serikali na sekta binafsi kupata rasilimali fedha za kugharamia miradi ya maendeleo, kuongezeka kwa akiba hapa nchini pamoja na kupanuka kwa uwekezaji unaoleta ongezeko la ajira.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com