MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi matofali 1,250 yenye thamani ya Shilingi Milioni mbili ikiwa ni jitihada zake za kuunga mkono wananchi wa vitongoji vya Ikugha na Daghusa zake uanzisha shule ili kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.
Akikabidhi matofali hayo ,Mtaturu amesema hizo ni jitihada zake za kusaidiana na serikali katikak uhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kusomea.
“Niombe Mkurugenzi atuletee mhandisi hapa kwa ajili ya kuchimba msingi haraka na mimi nitatanguliza mifuko 10 ya saruji ,Mwenyekiti unajua nahangaika na nini,nahangaika na matomaso ambao wao hawaamini mpaka waguse au waone,
“Hao watu wapo na wanatuchelewesha sana kufika tunapotaka kufika,wao wanategemea shule imwagwe hapa ikiwa imekamilika hapana lazima ianze na msingi, hivyo mimi nashughulika na matomaso,”amesema Mtaturu.
Social Plugin