MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki mahafali ya Shule ya Sekondari ya Mang’onyi Shanta na kugawa vifaa vya TEHAMA ikiwemo Printa na Kompyuta vyenye thamani ya Sh Milioni 13 ikiwa ni jitihada zake za kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katikak uboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Pamoja na kushiriki mahafali hayo pia ameanzisha upya ujenzi wa maabara za sayansi tatu zilizokwama tangu mwaka 2012 kwa kuchangia tofali 1,000 na mifuko ya saruji 100.
Akizungumza katika mahafali hayo Octoba 12,2023,Mtaturu amesema kazi yake ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma katika sekta zote na huduma hiyo ni pamoja na kuwatembelea na kujua changamoto zao ili uwe sehemu ya kuzitatua.
“Leo nimeona nije niungane nanyi ili na mimi niwe sehemu ya kuongeza taaluma shuleni hapa kwak ujibu kwa vitendo risala yenu,katika jambo nimefurahi leo ambalo limekuwa kiu yangu ya muda mrefu ni kuhakikisha watoto wanapata lishe mashuleni,kitendo hiki kitaongeza ufaulu maana utulivu utapatikana na umakini utakuwepo lakini pia walimu watapata muda wa kupanga ratiba yao vizuri,hongereni sana wazazi,walezi na walimu kwa kuamua kuwa na jambo hili,”.amesema.
Amesema Rais Samia amefanya kazi kubwa na anatamani watu wote wafanikiwe lakini miundombinu ndio inaweza kuwachelewesha hivyo amewahakikishia kushirikiana nao kwa ajili ya kuwezesha kuwa na chumba maalum cha kufundishia watoto.
“Ujio wangu hapa ni kuja kuwahakikishia kwamba tutaendelea kuboresha miundombinu na mimi kwa miaka miwili na nusu ijayo bado ni mbunge wa jimbo hili la Singida Mashariki hivyo nitaendelea kupiga kelele bungeni kuhakikisha tunapata madarasa ya kutosha,tunapata maabara ili Mang’onyi ibaki na heshima yake ya kuwa shule kubwa,
“Yaani leo ukifungua kitambaa Unyahati na Ikungi halafu ukamfunga tena akabebwa akasafirishwa hadi hapa Mang’onyi ukimfungua hataamini kama hii shule ipo Wilaya ya Ikungi ,haya ni matokeo ya siasa chafu tulizoziendekeza kwa miaka 10,leo hasara ni yetu wenyewe maana hao waliotudanganya watoto wao hawasomi hapa,tumekula chuya kwa uvivu wa kuchagua,”ameongeza.
Akisoma taarifa ya shule,Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mohammed Msafiri amesema wamefanikiwa kuwezesha wanafunzi kupata lishe shuleni na hivyo kuwa na ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo.
“Hapa tuna changamoto ya upungufu wa madarasa ,maabara zote tatu,hosteli za wanafunzi,ukumbi wa shule,vifaa vya TEHAMA,majisafi na salama na matundu ya vyoo,nimshukuru Mbunge Mtaturu kwak utupatia vifaa vya michezo vilivyochochea michezo shuleni hapa,”ameshukuru.
Diwani wa vitimaalum Fatuma Makula amempongeza mbunge kwa kazi kubwa anayofanya kwenye jimbo hilo kwani miradi ni mingi sana.
Social Plugin