Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa akiagana na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika ofisi hiyo Meja Jenerali Charles Mbuge mara baada ya kumaliza muda wake wa utumishi katika ofisi hiyo.
|
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (wanne kutoka kushoto) Naibu wake, Bw. Anderson Mutatembwa (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika ofisi hiyo Meja Jenerali Charles Mbuge (wanne kutoka kulia) tarehe 04 Oktoba 2023 katika ofisi yake Jijini Dodoma.
|
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kushoto) akiagana na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika ofisi hiyo Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) mara baada ya kumaliza muda wake wa utumishi katika ofisi hiyo.Ameagana naye tarehe 04 Oktoba 2023 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma. |
|
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto) Pamoja na Naibu wake Bw. Anderson Mutatembwa (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika ofisi hiyo Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati) mara baada ya mazungumzo yao ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa utumishi katika ofisi hiyo. |
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin