Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi akikabidhi Tuzo kwa waajiri ambao wamekua wakilipa michango ya waajiriwa wao kwa wakati.
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 Blog
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi ametumia hafla ya kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kuwakumbusha mamalishe Bodaboda na wajasiriamali kujiunga Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 6,2023 wakati wa kufunga wiki ya huduna kwa wateja Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga Amina Mdabi amesema wananchi wanapaswa kutumia Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kujiwekea fedha kidogo kidogo ili fedha hizo ziweze kuwasaidia siku za baadaye.
Pia Meneja Mdabi ametumia hafla hiyo kutoa tuzo kwa waajiri ambao wamekuwa wakilipa michango ya waajiriwa wao kwa wakati.
Social Plugin