Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja,akizungumza katika kongamano la Maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa Babati Mkoani Manyara.
..........
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Ofisi hiyo inatarajia kuandaa mtandao wa vijana nchi nzima ambao utaratibu masuala yanayo wahusu vijana.
Mtandao huo utakuwa na Maafisa vijana wa Wilaya na Mikoa ambao watahusika katika kutoa taarifa zinazohusu vijana zikiwemo fursa zinazotolewa na serikali, Taasisi na mashirika.
Mhandisi Luhemeja amebainisha hayo Oktoba 11, 2023 Babati Mkoani Manyara katika kongamano la Maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa ambapo amesema amesema lengo la Serikali ni kuona vijana wana mtandao mmoja ambao unarahisisha kuwafikia kwa wakati.
Amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameweka mazingira wezeshi kwa vijana ambayo yanampa fursa ya kujikwamua kiuchumi, hivyo wajitambue, wajitume, wafanye kazi kwa weredi na ubunifu serikali itawaunga mkono.