Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini wameadhimisha wiki ya UWT katika kata ya Usanda,kwa kutembelea kituo cha kulelea wazee cha Busanda kilichopo katika Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kutoa zawadi za vitu mbalimbali katika kituo hicho pamoja na kufanya usafi katika Zahanati ya Usanda na kuwapatia mahitaji muhimu kinanama waliojufungua katika wodi ya wazazi iliyopo katika Zahanati hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya UWT.
Umoja
wa Wanawake wa CCM UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini wametoa msaada huo
jana Oktoba 28, 2023 walipotembelea katika kituo cha kulelea wazee cha Busanda kilichopo katika Kata ya
Usanda halmashauri ya wilaya ya wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya wiki ya UWT , ambapo Wilaya ya Shinyanga Mjini imeadhimisha kwa kushiriki
katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi katika Zahanati ya
Usanda na kutoa mahitaji muhimu kwa akina mama waliojifungua katika zahanati
hiyo.
Baada ya kutoa zawadi za vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee Busanda na kufanya usafi na kukabidhi zawadi kwa akina mama waliojifungua pia wamefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Usanda na kuwahamasisha wanawake kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kutoa elimu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wananchi.Mjumbe wa Baraza kuu UWT Taifa Ndugu Christina Gule akiwa na viongozi wa UWT wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee Busanda
Social Plugin