Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MLOGANZILA YAANZISHA HUDUMA YA KUREKEBISHA MUONEKANO WA MWILI


Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza nchini itafanya huduma za kibingwa bobezi za upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi (Bariatric and Reconstructive surgery) kuanzia tarehe 27.10.2023.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji Dkt. Eric Muhumba amesema upasuaji huo utafanywa na wataalamu wa MNH-Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa kupunguza uzito na Upasuaji Rekebishi kutoka India, Dkt. Mohit Bhandari pamoja na MedINCREDI.

Dkt. Muhumba ameongeza kuwa huduma hizo za kupunguza uzito zinafanyika kwa kupunguza nafasi ya kuhifadhi chakula kwa kushona sehemu ya eneo la tumbo kitu kitakachosababisha mtu kutumia kiasi kidogo cha chakula hivyo kupunguza uzito.

Dkt. Muhumba amebainisha kuwa katika kutoa huduma hizo watatumia njia ya kisasa ambayo haitahusisha upasuaji ambapo watatumia kifaa maalumu kiitwacho endoskopia kuingia katika tumbo na kupunguza nafasi ya tumbo la chakula.

“Upasuaji huu utafanyika kwa bei nafuu sana ukilinganisha na endapo mtu angeenda kutafuta huduma hizi nje ya nchi, hivyo tumeamua kuwasogezea wananchi huduma hizi na kuwapunguzia usumbufu wa wananchi kusafiri nje ya nchi kutafuta huduma hizi”Amesema Dkt. Muhumba

Sambamba na huduma hizo Dkt. Muhumba ameongeza kuwa huduma rekebishi itahusisha kurekebisha kwa kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu ya mwili mfano kupunguza au kuongeza ukubwa wa matiti, nyama kwenye mikono na sehemu nyingine mbalimbali za mwili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com