Na Mwandishi Maalum,Dodoma
Mwenge wa Uhuru ambao uko Mkoani Dodoma kwa siku ya tano sasa umefika katika Wilaya ya Chamwino na kumulika Miradi mbalimbali ikiwemo Miradi ya Maji na Elimu, kutembelea na kujionea vijana wa kikundi cha ELLYDIZDON wanavyofanya kazi za uzalishaji na utengenezaji bidhaa kupitia Aluminium pamoja na kutembelea shamba la Mwekezaji wa kilimo (Mtimbi Farm).
Hata hivyo Mwenge wa Uhuru umepita na kutembelea mabanda mbalimbali yanayotoa Elimu za Lishe, Rushwa, Ukimwi na magonjwa Mengine mbalimbali.
Suala la Utunzaji Mazingira limekuwa likipewa kipaumbele na viongozi mbalimbali wa Kitaifa hivyo Mwenge wa Uhuru umetembelea Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira katika kitalu cha Miti Ikowa ambapo wakimbiza Mwenge Kitaifa na viongozi mbalimbali walipata fursa ya kupanda Miti katika Eneo Hilo.
Wilaya ya Chamwino Imepata hati Safi baada ya Miradi yote kukidhi vigezo vya ubora unaotakiwa.
Leo Octoba 5,Mwenge wa Uhuru utakuwa Wilayani Mpwapwa na kesho 05/10/2023 utaelekea Wilayani Kongwa ambapo itakuwa ndio kilele cha Mwenge wa Uhuru Mkoani Dodoma.