Watumishi wa NEMC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Kituo cha Sayansi na Mazingira (Centre for Science and Environment) kutoka India mara baada ya kupata uelewa kuhusu masuala ya ukaguzi wa Mazingira . Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 16,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam
*************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC) wamezindua mwongozo wa ukaguzi binafsi wa mazingira yenye lengo la kukagua maeneo ya Uwekezaji na Taasisi binafsi ambayo itawasaidia kujua mambo ya kuzingatia katika uhifadhi mazingira yao.
Akizungumza Oct 16,2023 wakati wa uzinduzi huo uliombatana na mkutano wa kubadirishana Ujuzi na CSE ya India Mkurugenzi wa NEMC,Dkt.Samuel Gwamaka amesema wamekuwa na ushirikiano mzuri na India katika kujenga uwezo wa wafanyakazi wa NEMC katika kutunza mazingira.
"Wametusaidia Sana katika kutunza mazingira, kuna watumishi wetu walienda India na kupata mafunzo mbalimbali ya kutunza mazingira yetu,wametusaidia kufanya tafiti huko ziwa Victoria kuhakikisha ikolojia ya Ziwa Victoria inabaki kudumu na maji yataendelea kuwa bora, na kuonesha namna tunavyoweza kukusanya taka ngumu na kuzihifadhi"amesema
Aidha Dkt.Gwamaka amesema kifungu Cha 18,1A na kifungu Cha 101 Cha Sheria ya Mazingira cha mazingira kinasema kila kiwanda kinaweza kufanya ukaguzi binafsi na NEMC imepewa mamlaka ya kukagua mazingira endapo wataona Sheria za ufadhi zimekiukwa.
"Muongozo mpya. uliozinduliwa unatoa picha ya pamoja kwa wataalamu wa mazingira wanapofanya ukaguzi wa mwaka ni mambo gani ya msingi yanapaswa kuzingatiwa hivyo sasa mazingira yetu yanakwenda kuwa safi na bora zaidi "amesema
Kwa upande wake mmoja wa wawakilishi kutoka India amesema wao wameshiriki Katika kuandaa ripoti ya utafiti wa mazingira na kuandaa mwongozo wa utunzaji mazingira katika Ziwa Victoria.
"Miaka miwili iliyopita Kituo cha Mazingira na Sayansi kiliamua kufanya utafiti ziwa Victoria Tanzania ni nini kinapelekea uchafuzi unaoharibu ziwa Victoria na njia gani za kusafisha ziwa Victoria na kuto ripoti ya utafiti huo"amesema.
Uzinduzi huo umeambatana na Mafunzo kwa watumishi wa NEMC na wadau mbalimbali wa mazingira.
Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC) wakiongozwa na Mkurugenzi wa NEMC,Dkt.Samuel Gwamaka wakiwa pamoja na wawakilishi wa Kituo cha Sayansi na Mazingira (CSE) kutoka India wakionesha mwongozo wa ukaguzi binafsi wa mazingira yenye lengo la kukagua maeneo ya Uwekezaji ambayo itawasaidia kujua mambo ya kuzingatia katika uhifadhi mazingira yao wakati wa uzinduzi wa mwongozo huo leo Oktoba 16,2023 kwenye Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC), ,Dkt.Samuel Gwamaka (kushoto) akipongezana na Mwakilishi wa Kituo cha Sayansi na Mazingira (CSE) kutoka India wakipongezana mara baada ya uzinduzi wa mwongozo wa ukaguzi binafsi wa mazingira yao uliofanyika leo Oktoba 16,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC), ,Dkt.Samuel Gwamaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa ukaguzi binafsi wa mazingira yenye lengo la kukagua maeneo ya Uwekezaji ambayo itawasaidia kujua mambo ya kuzingatia katika uhifadhi mazingira yao uliofanyika leo Oktoba 16,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Kituo cha Sayansi na Mazingira (CSE) kutoka India (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa ukaguzi binafsi wa mazingira yenye lengo la kukagua maeneo ya Uwekezaji ambayo itawasaidia kujua mambo ya kuzingatia katika uhifadhi mazingira yao uliofanyika leo Oktoba 16,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Social Plugin