NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Rehema Kasim Muhina akizungumza wakati wa kikao cha kuhitimisha mradi wa usalama barabarani kupitia Tanga Yetu uliokuwa ukiendeshwa na Shirika la Amend Tanzania chini ya Ufadhili Shirika la Botnar Foundation ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2023, kuhusiana na suala zima la usalama barabarani.
NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Rehema Kasim Muhina akizungumza wakati wa kikao cha kuhitimisha mradi wa usalama barabarani kupitia Tanga Yetu uliokuwa ukiendeshwa na Shirika la Amend Tanzania chini ya Ufadhili Shirika la Botnar Foundation ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2023, kuhusiana na suala zima la usalama barabarani.
Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mradi huo
Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mradi huo
Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mradi huo
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga Shadia Ally akieleza namna walivyonufaika kupitia mradi huo
Sehemu ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakiwa kwenye kikao hicho
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho
NAIBU meya wa Jiji la Tanga Rehema Kasimu kushoto akimpatia cheti cha kutambua mchango wa Mwalimu wa Shule ya Msingi Usagara Faraja Mwajike kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya usalama barabarani mapema leo
Na Oscar Assenga, TANGA
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga limelishukuru Shirika la Amend Tanzania kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu usalama barabarani sambamba na uboreshaji wa miundombinu katika shule za Msingi hatua iliyowezesha kupunguza ajali
Elimu hiyo ilitolewa kupitia mradi wa Usalama Barabarani kupitia Tanga Yetu chini ya Ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika rasmi mwaka 2023 ambao umekuwa na manufaa makubwa.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mradi huo ambao ulianza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2023, Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow amesema katika kipindi cha miaka minne wamekuwa na Amend katika kushirikiana kuhusiana na suala zima la usalama barabarani.
“Amend ni miongoni mwa mashirika yanayofanya kazi kwa ukaribu katika program ya Tanga Yetu , ni miongoni mwa miradi 17 tuliyokuwa nayo katika miradi ya Tanga Yetu na moja ya mradi huo ni mradi wa usalama barabarani.Katika mradi huu waliokuwa wamepata kazi ya kuusimamia na kuendesha ni Amend.
“Mradi huu umefika mwisho na umefanyika kwa miaka minne ukiwa unafadhiliwa na Shirika la Botnar chini ya mradi wa Tanga yetu na leo tumekuja kuwapa taarifa wadau tuliokuwa tunashirikiana nao tangu mwanzo kama.
“Ni mradi ambao umekuwa na mafanikio makubwa ndani ya miaka hii minne kwa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani imetengamaa na imejitosheleza katika jiji letu la Tanga, kwasababu mradi huu pia uligusa uboreshaji wa miundombinu,”amesema Shiloow.
Amefafanua wameboresha miundombinu katika Shule ya Msingi Usagara, Shule ya Msingi Chuda, Shule ya Msingi Mwazange na Shule ya Msingi Mabawa. “Tumeboresha miundombinu hii ambayo imetengenezwa maeneo mahususisi ambayo watoto wanaweza kupita kwa usalama na kuepuka kupata ajali za barabarani.
“Lakini kuweka alama za barabarani, tumeweka matuta, kingo, zebra na alama mbalimbali za kuashiria watumiaji wa vyombo vya moto kwamba wako katika maeneo ya shule.Amend pia wametoa elimu kubwa kwa watoto wa shule za msingi, sekondari, madereva wa bodaboda, maofisa wa maendeleo ya jamii , askari wa kikosi cha usalama barabarani.
“Elimu hiyo imetolewa ya kutosha katika Jiji la Tanga na zimetolewa kwa nyakati tofauti lakini hawakuishia hapo wametoa elimu kwa madereva zaidi ya 900 ambao nao walipewa elimu sahihi ya matumizi ya barabara lakini jinsi gani ya kumlinda mtumia barabara ili na yeye awe salama.”
Ameongeza kikubwa zaidi ambacho Amend walikifanya na kuvutia zaidi ni kuwa kuanzisha Mahakama Kifani ya Watoto iliyokuwa ikiendesha kesi za madereva waliovunja sheria za usalama barabarani na madereva hao walihukumiwa.
Meya Shiloo amesema Mahakama ya Watoto imewasaidia watoto hao kuwa na ujasiri na kufahamu haki zao kuwa sheria za barabarani zipo na zinatakiwa zifuatwe na zinaweza kutolewa hukumu na watu wakahukumiwa.Pia amesema kupitia mradi huo kumekuwepo na mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uelewa wananchi.
“Tunawashukuru Amend walitutengenezea mpango kazi wa Jiji letu la Tanga kuhusu suala zima la usalama barabarani, ni suala kubwa kwetu .Niwaambie tu Amend wamekuwa na sisi kwasababu tu ya kufadhiliwa na Fondation Botnar na sasa mradi umekwisha.
“Jambo la kufurahisha mradi huu umekwisha lakini Amend wamepata mfadhili mpya ambaye ni Serikakali ya Uswiss ambao wameona umuhimu wa kuendelea na Amend katika Jiji la Tanga pamoja na Jiji la Dodoma ambako nako watapata huduma kama ambazo zimetolewa kwetu.
“Amend wanafanya kazi kwa uhalisia na linafanya kazi na watu wenye uhitaji, watu ambao wanahitaji kusemewe na sisi kama viongozi wa umma tunawasemea watoto wetu ili tujenge taifa nzuri lisilokuwa na watoto wenye ulemavu kwa miaka ijayo na ili tujenga taifa lenye upendo ni lazima tuwajali hawa watoto ikiwa pamoja na kuangalia usalama wao,”amesema Shiloow.
Awali akizungumza katika kuhimitisha mradi huo Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo alisema mafanikio tokea kuanzishwa mradi huo mwaka wa 2019 wamefanya kazi mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika shule za msingi 11.
Alisema katika uboreshaji huo ulikuwa ni pamoja na njia za miguu, madaraja ya waenda kwa miguu, alama za barabarani, matuta, alama za pundamilia, na zaidi;
Meneja huyo alisema pia walitoa mafunzo kwa waendesha pikipiki kwa waendesha pikipiki zaidi ya 900, kwa kushirikisha Polisi wa Trafiki na viongozi wa vyama vya bodaboda;
“Lakini pia utekelezaji wa Mahakama ya Watoto katika shule tano za msingi (Usagara, Mwanzange & Martin Shamba, Mwenge, Mwakizaro),Elimu ya usalama barabarani kwa zaidi ya watoto 12,000 wa shule za msingi,Uwezeshaji wa mafunzo kwa Polisi wa Trafiki”Alisema Meneja huyo.
Alisema kwamba kampeni hiyo ya uhamasishaji wa usalama barabarani ilikuwa ikijumuisha kampeni ya vyombo vya habari, ujumbe kupitia kwa maafisa wa maendeleo ya jamii na ujumbe kupitia wanasiasa wakiwemo madiwani,
Warsha zaidi ya nane za wadau na wadau muhimu zikiwahusisha wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mkurugenzi wa Jiji na Mkurugenzi, Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani.
Jumla ya maofisa wa serikali 139, taasisi za elimu 14, wanafunzi 12,894, walimu 128, askari polisi 29 na madereva 1,220 wameguswa moja kwa moja na mradi huu.
Kutengeneza Mpango Kazi wa Usafiri Salama na Endelevu wa Jiji la Tanga.
Awali akizungumza Naibu Meya wa Jiji la Tanga alilishukuru Shirika la Amend Tanzania kwa usimamizi na utekeleza mzuri wa mradi huo ambao umekuwa na tija kubwa kwa kuwezesha kupunguza ajali zilizokuwepo awali.
Alisema kwamba Amend wamewatenda haki na waliyoyafanya yanaonekana na hivyo kuhakikisha usalama kwa watoto wa Tanga wanakuwa salama wakati wanapotumia barabarani kwenda shuleni na kurudi nyumbani
“Lakini pia niwapongeze Botnar kwa kujali watoto kwa kufadhili mradi huo miaka minne na kufadhili miradi 17 kwa jiji la Tanga ambayo imelenga kuboresha mazingira ya watoto na vijana na kuwajengea vijana uwezo ili wasiwe kuajiriwa bali wajiajiri “Alisema
Hata hivyo alisema miradi hiyo imekuwa na matokeo makubwa sana yanayoonekana, na shughuli hizo zimeweza kupunguza ajali kwa watoto huku akieleza jukumu la Amed wamefanya ya muhimu katika kuboresha miundombinu ambayo imehakikisha usalama kwa watoto .
“Nitoe rai kwa watu wote kuendelea kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabara kwa watumiaji, kuheshimu vivuko vya watembelea kwa miguu vilivyopo hata kwa waendesha pikipiki,uvaaji kofia ngumu kwa waendesha pikipik kwao na abiri”Alisema
Hata hivyo alisema kutokana na uwepo wa mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali kutokana na maboresha hayo hivyo ni taarifa njema huku akiwataka wasibweteke waendelee kuhamasisha matumizi salama ya barabara kwa Jiji la Tanga
Social Plugin