Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA AL AHLY MICHUANO AFL


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imefanikiwa kutoka sare ya 2-2 katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya timu ya Al Ahly ya nchini Misri katika mchezo wa robo fainali Michuano ya African Football League.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa ufunguzi, Al Ahly ilifanikiwa kupata bao kipindi cha kwanza kabla ya mapumziko kupitia kwa mshambuliaji wao Reda Slim na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 1-0.

Simba Sc ilirudi kipindi cha pili wakiwa na hali mpya kwani walitawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kibu Denis dakika ya 53 ya Mchezo.

Kocha wa Simba Sc alifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji kipindi hicho cha pili, mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwani baada ya kuingia Sadio Kanoute alifanikiwa kupachika bao zuri na kuwafanya Simba kuwa mbele 2-1.

Dakika tatu baadae Al Ahly walisawazisha kupitia kwa nyota wao Karhaba dakika ya 63 ya mchezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com