Na Mwandishi Wetu Dodoma
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi *Fakii Raphael Lulandala (MNEC)* amesema Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi unalo Jukumu la kukilinda Chama cha Mapinduzi na Viongozi wake kwa wivu mkubwa bila kuogopa mtu yoyote.
Ameyasema hayo wakati anahutubia wananchi Mkoani Dodoma mara baada ya Mapokezi yake yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya UVCCM Dodoma tarehe 04 Oktoba, 2023.
"Kutakua hakuna sababu ya kuwa na Katibu au Mwenyekiti wa UVCCM kwenye Wilaya zetu, kata zetu na Mikoa kama Chama cha Mapinduzi kinashambuliwa katika maeneo yao, Ukiona Mchungaji wa kondoo amepigwa lengo sio mchungaji ni kondoo" alisema Komredi Lulandala.
Aidha Komredi Lulandala amesema viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi lazima kuwa mfano kuwatetea viongozi na kukilinda Chama cha Mapinduzi.
Amesema kupambana na hoja za wapotoshaji na walaghai ni agenda ya kudumu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi.
"Suala la Kupambana na hoja za wapotoshaji na walaghai ni agenda ya kudumu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi". Alisema Komredi Lulandala