Na Dotto Kwilasa,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Oktoba 05, 2023 amewaaga Kikundi cha Waendesha baiskeli (TWENDE BUTIAMA) kinacho husisha vijana Wapanda baiskeli 73, wanne Kati Yao wakiwa wanawake kutoka Mikoa 10 ya Tanzania bara ,Zanzibar .
Aidha wengine ni kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na kudhaminiwa na taasisi ya VODACOM FOUNDATION TANZANIA kwa ajili ya safari ya kuelekea Wilaya ya Butiama Mkoani Mara. Hafla imefanyika katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Akiwaga waendesha baiskeli hao Mhe. Senyamule amesema lengo la msafara huo nikuendelea kumuenzi Baba kwa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere kwa Vitendo kupitia Kampeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha elimu, afya na kutunza Mazingira.
Aidha, Katika kuendelea kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kikundi hicho kimefanikiwa kupanda idadi ya miti 500 na kugawa madawati 70 katika Shule ya Msingi Medeli A iliyopo pamoja na baiskeli 27 Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Awali Msafara huo umeanzia Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na unaendelea Singida, Igunga, Nzega, Shinyanga, Mwanza, Ukerewe, Bunda, Musoma na kuishia Butiama tarehe 14 Octoba,2023 ambapo ndio kilele chake cha siku ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Social Plugin