ULOWA BINGWA CHEREHANI CUP 2023.....RAIS SAMIA APEWA TANO KUIMARISHA MICHEZO







Na Mathias Canal, Ushetu-Shinyanga

Mashindano ya CHEREHANI CUP 2023 yamefika ukomo tarehe 15 Ok

toba 2023 katika uwanja wa Nyamilangano yakiwa yamefanyika kwa zaidi ya wiki tatu huku jumla ya timu 20 kutoka kata zote za Halmashauri ya Ushetu zikiwa zimeshiriki.

Katika mashindano hayo timu ya Ulowa Fc kutoka kata ya Ulowa imeibuka kidedea baada ya ushindi wa goli 2 kwa 0 dhidi ya timu ya Ukune kutoka kata ya Ukune.

Mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndg Mabala Mlowa amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe Dkt Emmanuel Cherehani kwa kuanzisha na kudhamini mashindano hayo ambayo yana leongo la kuimarisha sekta ya michezo na uimarishaji wa afya kwa vijana.

Pia amemwomba mdhamini huyo kuongeza timu na michezo mingine hususani itakayohusisha wanawake. "Na mimi nataka niwaambie tu kuwa 2025 uchaguzi Ushetu mlishamaliza kwa sababu ilani ya CCM inatekelezwa mnataka tumlete nani tena zaidi ya Mbunge wenu Cherehani" Amehoji Ndg Mlowa

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mashindano hayo Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga Mhe Emmanuel Cherehani amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha sekta ya michezo nchini hususani mpira wa miguu.

Amesema kuwa wabunge wamepata nguvu ya kuanzisha mashindano mbalimbali katika majimbo yao kwa kumuunga mkono Rais kutokana na uwekezaji na hamasa yake katika michezo.

Mhe Cherehani amesema kuwa jumla ya michezo 33 imechezwa katika mashindano hayo ambapo jumla ya wachezaji 33 watatangazwa kutoka kata zote 20 za Halmashauri kwa ajili ya kuunda timu ya jimbo hilo.

Amesema kuwa mechi zilichezwa katika mizunguko sita na mtoano, kwenye mizunguko kila timu ilicheza nyumbani na ugenini huku ligi hiyo ikichezwa katika viwanja vya kata zote.

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndg Odilia Abraham amesema kuwa katika mashindano hayo hapakuwa na mshindi bali kuna timu iliyoongoza hivyo amewatoa hofu waliopoteza kombe hilo kwa kutolewa mapema na kutoshiriki fainali na kiwataka kujiandaa vizuri katika mashindano mengine.

Ndg Odilia amesema kuwa Michezo ni afya, michezo ni Upendo, michezo ni Amani, michezo ni mshikamano kadhalika michezo ni ajira hivyo vijana wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na serikali kupitia sekta ya michezo kwani huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post