WANAWAKE kutoka vikundi na maeneo tofauti tofuati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Dar es Salaam wameanza safari leo hii kuelekea Dodoma kwaajili ya mapokezi ya kukabidhiwa ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Jokate Mwegelo.
Jokate ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Oktoba 12 mwaka huu anatarajiwa kukabidhiwa ofisi mjini Dodoma , hivyo wanawake hao walioanza safari leo wanatarajia kuungana na wanawake wengine kufanikisha mapokezi hayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanawake kwa umoja wao wamesema wanamshukuru Rais ambaye ni Mwenyekiti CCM Taifa, kuwateuliwa Katibu Mkuu kijana lakini ni mwanamke mwenzao, wanamuanini Jokate Mwegelo na kubwa zaidi ni mpenda maendeleo.
"Jokate Mwegelo anapenda sana maendeleo, jumuiya yetu sasa inaenda kuwa ya mfano katika Chama chetu, sisi kama wanawake tumeungana kwa pamoja kuhakikisha Dodoma tunakua moto” amesema Hawa Abdulrahaman ambaye ni Diwani Viti Maalum Ubungo
Social Plugin