Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog
Wakati Mashindano ya Dkt. Samia Cup yakiendelea
kutimua vumbi katika viunga mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kwa lengo la kumtafuta bingwa atakayeibuka na zawadi mbalimbali
katika mashindano hayo,Timu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCC)
kata ya Ngokolo imekubali kutolewa kibabe na Timu ya Tanroads (Rangers fc )kutoka
Tanroads katika Mtanange uliopigwa
katika uwanja wa Chuo cha ualimu Shinyanga (Shy Com) ikiwa ni hatua ya kutafuta
timu zitakazo shiriki hatua ya Fainali
Katika mchezo huo Timu ya UVCCM Ngokolo imeshindwa kutamba mbele ya Timu ya Tanroads (Rangers fc ) kutoka Tanroads baada ya kukubali kufungwa goli moja kwa sifuri na Timu ya Tanroads (Rangers fc katika mashindano hayo huku Tanroads ikipata tiketi ya kwenda kushiriki katika hatua ya fainali.
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA, Jackline Isaro, akitazama burudani
Kocha wa timu ya Tanroads (Rangers ) akikochi vijana wake.
Kocha wa timu ya Ngokolo akikochi vijana wake
Viongozi wakifuatilia mashindano ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA
Social Plugin