Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANYAMAPORI HAI WANOGESHA MAONESHO YA UTALII MWANA KATAVI



Na Beatus Maganja 

Wanyamapori hai wametajwa kuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya Utalii  Mwana Katavi yanayofanyika wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi kiasi cha kufanya wakazi wa Mkoa huo kufurika katika banda la TAWA ili kupata maelezo kuhusu tabia na fursa za ufugaji wa Wanyamapori hao.

Maonesho haya ambayo hufanyika Kila mwaka Mkoani humo yalifunguliwa rasmi Oktoba 25, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko ambapo leo  Oktoba 31, 2023 yanatarajiwa kufikia tamati.

 TAWA imeshiriki na kutumia maonesho hayo kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwahimiza wakazi wa Mkoa huo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo ukanda wa magharibi hususani bustani ya Wanyamapori hai Tabora almaarufu Tabora ZOO iliyo chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA

Wanyamapori waliokuwa kivutio katika maonesho hayo ni Simba, chui, fisi, Kobe na ndege wa aina mbalimbali ambao walichochea udadisi wa uelewa kwa wanafunzi wa shule za awali na sekondari waliotembelea banda la TAWA 

TAWA inaendelea kutumia vyema maonesho mbalimbali yanayofanyika ndani na nje ya nchi yetu kunadi fursa za utalii na  uwekezaji zilizosheheni katika taasisi hii ili kuchangia katika lengo la Serikali kufikisha idadi ya  watalii Millioni Tano (5) ifikapo 2025

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com