Hali ya taharuki imetokea katika eneo la Kihonda kwa Chambo Manispaa ya Morogoro mara baada ya wakazi wa maeneo hayo kukuta watoto mapacha wanaokadiriwa kuwa na umri wa siku moja wakiwa wametupwa porini huku miili yao ikiwa kwenye mfuko.
Tukio hilo limetokea leo Oktoba 13, 2023 Manispaa na Mkoa wa Morogoro na kuibua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.
Wakizungumza na vyombo vya habari mashuhuda wa tukio hilo wamelaani kitendo hicho cha watoto hao mapacha kutupwa porini wakiwa wamepoteza maisha huku wakisema kuwa tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika eneo hilo.
Tayari miili ya watoto hao imechukuliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi ambapo Jeshi hilo limeahidi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo.
Social Plugin