Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA WANANCHI ELFU 36 WANAPATA MAJI KWENYE MRADI WA MAJI MBINGU - IGIMA IFAKARA

 



Na Mwandishi Maalam. 

Kamati ya Bodi ya Miradi na Ufundi ya RUWASA inaendelea na ziara Mkoani Morogoro. 

Leo Kamati imetembelea Mradi wa maji Mbingu - Igima unaonufaisha zaidi ya wananchi elfu 36 wa Vijiji saba katika kata za Mbingu na Igima, Tarafa ya Mngeta Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero.

Kazi zilizofanyika kwa awamu ya kwanza ni pamoja na Ujenzi wa Dakio la maji (Intake), Ulazaji wa bomba za maji zenye urefu wa mita 22,313, Ujenzi wa Chujio la maji (sedmentation tank, Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Lita 250,000 juu ya ardhi na Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 20. Bado kazi zinaendelea kwa awamu ya pili na tatu.

Gharama za mradi mpaka kukamilika kwake ni shilingi 3,431,773,992.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com