Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

EWURA YAELIMISHA WAANDISHI WA HABARI TABORA KUHUSU UDHIBITI




Meneja Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya EWURA kwa wajumbe wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Tabora katika semina ya kuwajengea uwezo iliyofanyika mjini Tabora leo 22 Novemba, 2023.

Na.Mwandishi Wetu-TABORA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), leo 22 Novemba 2023, imewajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa wa Tabora kuhusu kazi na majukumu ya EWURA.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bwana Titus Kaguo amewaeleza waandishi hao kuwa, EWURA hutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya EWURA, Sura Na 414 ya sheria za Tanzania sanjari na kuzingatia sheria za sekta inazozidhibiti za nishati na maji.

“ EWURA imekuwa ikidhibiti sekta za nishati na maji kwa mujibu wa sheria na kwa kipindi cha miaka 17 sasa, utendaji wa Mamlaka umekuwa na tija kwenye jamii, tumetoa leseni kwa mafundi umeme, tumedhibiti uchakachuaji wa mafuta, tumefungua fursa za vituo vya mafuta vijijini na tumehakikisha ubora wa maji yanayotumika majumbani” Alisema.

Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Walter Christopher, ametumia fursa hiyo kuitambulisha ofisi ya Kanda, ambapo ameeleza itatoa huduma kwenye mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi na Shinyanga.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Tabora, Juma Kapipi ameishukuru EWURA kwa kuwajengea uwezo baada ya Klabu hiyo kuiomba EWURA kutoa elimu, hatua ambayo EWURA iliridhia na kuwakutanisha kwa ajili ya mafunzo ya siku moja.


Meneja Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya EWURA kwa wajumbe wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Tabora katika semina ya kuwajengea uwezo iliyofanyika mjini Tabora leo 22 Novemba, 2023.


Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Tabora, Juma Kapipi ( kulia) akifurahia jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo, wakati wa semina kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji kwa waandishi wa habari wa mkoa huo, leo 22 Novemba 2023.



Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Walter Christopher akitambulisha ofisi ya Kanda kwa wajumbe wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Tabora, wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya udhibiti, mjini Tabora leo 22 Novemba 2023


Baadhi ya Waandiashi wa Habari wakifuatilia mada wakati wa semina kuhusu masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji, mjini Tabora leo 22 Novemba 2023.



Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Titus Kaguo (wa tano kutoka kulia) na Kaimu Meneja EWURA, Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher (wa kwanza kulia mstari wa mbele), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Tabora, wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo waandishi hao kwenye masuala ya Udhibiti iliyofanyika leo 22/11/23 mjini Tabora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com