VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA VYAWASILISHA HOJA KWENYE KAMATI YA FEDHA HALMASHAURI YA KISHAPU MAAZIMIO TAMASHA LA JINSIA... 'WAKAZIA VYUMBA MAALUM WANAWAKE KWENYE MASOKO, STENDI"

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Songwa wilayani humo Mhe. Abdul Ngoromole wameshiriki kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
na kuwasilisha hoja za masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na wanaharakati wa haki za wanawake wakati wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia (TGNP) na Tapo la Ukombozi wa Wanawake.

Vituo hivyo vya Taarifa na Maarifa vimewasilisha hoja zilizotokana na Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 TGNP leo Ijumaa Novemba 17,2023 kwenye kikao hicho baada ya Diwani wa kata ya Songwa, Mhe. Abdul Ngoromole kuomba awasilishe hoja mahsusi akiambatana na wanajamii kupitia vituo 9 vya taarifa na maarifa walioshiriki kwenye tamasha ili kuwasilisha mambo yaliyojadiliwa na kuwekewa maazimio kwa lengo la utekelezaji kwa serikali na halmashauri zake.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha hoja, Mhe. Ngoromole amesema katika tamasha hilo lililofanyika Novemba 7-10 Jijini Dar es salaam likihudhuriwa na wadau kutoka ndani na nje ya Tanzania mambo mbalimbali yalijadiliwa na kwa kuwa Halmashauri ni mdau mkubwa wa masuala ya mrengo wa kijinsia wameleta hoja nne miongoni mwa hoja kadhaa zilizoibuliwa kwa lengo la majadiliano na utekelezaji kwa manufaa mapana ya halmashauri na taifa kwa ujumla.

Mhe. Ngoromole ametaja miongoni mwa hoja hizo kuwa ni kukosekana kwa afua za kutosha katika ngazi ya halmashauri zinazojielekeza katika kutatua changamoto za masuala ya afya ya uzazi wa wasichana mashuleni na nje ya shule mfano elimu juu ya hedhi salama na usafi binafsi haitolewi kwa kiasi cha kutosha.

Ameeleza kuwa, afua hizo ni pamoja na kuangalia uwepo wa miundombinu yenye kuzingatia jinsia katika masoko na vyoo vinavyojengwa kwenye masoko na stendi za mabasi.

“Tulioshiriki kwenye tamasha la 15 la Jinsia tulikubaliana kuweka azimio kwenye Halmashauri zetu na kutaka kuzishawishi halmashauri kutengeneza miundombinu yenye kuzingatia jinsia katika masoko yetu tunakofanyia biashara pamoja na taasisi tunazoendelea kujenga kwenye taasisi za elimu ya msingi na sekondari, Zahanati na vituo vya afya pamoja na kujenga masoko, mfano sisi Kishapu tuna mpango wa kujenga Stendi ya Mabasi Maganzo na Soko Maganzo”,ameeleza Ngoromole.

“Mhe. Mwenyekiti tumeleta hoja hii binafsi tunaomba Kamati yako ya fedha iridhie kujenga chumba maalumu katika Stendi ya Maganzo na Soko la Maganzo kwa ajili ya kuhudumia wanawake kujistiri na kunyonyeshea watoto. Tunaiomba kamati ya fedha iridhie mapendekezo yetu haya na tutafurahi sana kuona yamebarikiwa na utekelezaji wake ukafanyike kwa ngazi ya jamii itakuwa heshima kwetu wana Kishapu”,ameongeza Mhe. Ngoromole.

Kwa upande wake, Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu Bi. Fredina Said ameyataja mambo mengine waliyopa kipaumbele yanayotakiwa kufanyiwa utekelezaji na halmashauri ni kuibuka kwa wimbi kubwa la ukatili na unyanyasaji wa watoto wa kiume ambapo suala hilo linapaswa liwe moja ya ajenda kuu za mapambano katika kumlinda mtoto wa kiume na wa kike.

“Hoja nyingine ni kukosekana kwa majukwaa ya kutosha ya wakulima hasa wakulima wanawake ambao wanazalisha mazao ya chakula kupaza sauti zao, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na matumizi makubwa ya mbolea na viuatilifu vya viwandani na uchafuzi wa mazingira imekuwa tishio kubwa kwa upatikanaji wa chakula salama”,ameeleza Fredina.

Hoja nyingine waliyowasilisha kwenye kikao hicho ni kuibuka kwa wimbi la mikopo kausha damu ambayo inaathiri zaidi uchumi wa wanawake na watu maskini ambapo suala hilo limekuwa changamoto kubwa kwenye halmashauri hiyo hali inayosababisha baadhi ya wanawake kukimbia familia zao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo amesema wajumbe wa kamati hiyo wamepokea hoja hizo na kwamba watazifanyia kazi.

“Hoja imepokelewa. Tunawashukuru Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kwa jinsi mnavyojitoa kushirikiana na serikali kushughulikia matatizo ya jamii, tunawashukuru kwa kuleta hoja hatutazibeza, tutazifanyia kazi”, amesema Mhe. Jijimya.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Diwani wa Kata ya Songwa wilaya ya Kishapu Mhe. Abdul Ngoromole akiwasilisha Hoja kuhusu masuala yaliyoibuliwa katika Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake leo Ijumaa Novemba 17,2023 kwenye Kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Diwani wa Kata ya Songwa wilaya ya Kishapu Mhe. Abdul Ngoromole akiwasilisha Hoja kuhusu masuala yaliyoibuliwa katika Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake leo Ijumaa Novemba 17,2023 kwenye Kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 

Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu Bi. Fredina Said akiwasilisha Hoja kuhusu masuala yaliyoibuliwa katika Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake leo Ijumaa Novemba 17,2023 kwenye Kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu 

Wanavituo vya taarifa na maarifa Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

Wanavituo vya taarifa na maarifa Kishapu na wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa ukumbini.
Diwani wa Kata ya Songwa wilaya ya Kishapu Mhe. Abdul Ngoromole na Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilaya ya Kishapu, Peter Nestory (kulia) wakionesha tuzo zilizotolewa kwa Vituo vya Taarifa na Maarifa Ukenyenge na Kiloleli wakati wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo (kulia) akipokea tuzo zilizotolewa kwa Vituo vya Taarifa na Maarifa Ukenyenge na Kiloleli wakati wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo (wa pili kulia) akipokea tuzo zilizotolewa kwa Vituo vya Taarifa na Maarifa Ukenyenge na Kiloleli wakati wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake
Wanavituo vya taarifa na maarifa Kishapu  wakipiga picha ya kumbukumbu na meza kuu kwenye kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Wanavituo vya taarifa na maarifa Kishapu na wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakipiga picha ya kumbukumbu
Wanavituo vya taarifa na maarifa Kishapu na wajumbe wa Kamati ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Diwani wa Kata ya Songwa wilaya ya Kishapu Mhe. Abdul Ngoromole (kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post