Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TGNP YAZINDUA ILANI YA MADAI YA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 NA UCHAGUZI MKUU 2025

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umezindua Ilani ya Madai ya wanawake katika uchaguzi (Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) yenye lengo la kudai mabadiliko ya mifumo kandamizi inayohalalisha ubaguzi wa wanawake katika uchaguzi kama wapiga kura, wenye kuwania nafasi za teuzi na hatimaye kuwakwamisha kwenye kuchaguliwa kama wawakilishi katika ngazi mbalimbali.

Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2025 'Ajenda ya Mwanamke, Turufu ya Ushindi'  imezinduliwa leo Ijumaa Novemba 10, 2023 wakati wa Hitimisho la Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake katika viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati akizindua Ilani ya Madai ya wanawake katika uchaguzi, Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na Usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena  ambaye ni Mwanachama wa TGNP amesema ilani hiyo inaendeleza madai ya wanawake watetezi wa haki za ushiriki katika uongozi wa kisiasa tangu nchi ilipopata Uhuru hadi leo.

"Hii ni Ilani ya sita ya madai ya wanawake katika uchaguzi. Ilani ya kwanza ilikuwa ya mwaka 2000 ikijulikana kama Ilani ya Wapigakura, ya pili ni ya mwaka 2005, ya tatu ni ya mwaka 2010, ya nne ni ya mwaka 2015 ya tano ni ya mwaka 2020. Maandalizi ya ilani zote sita yaliongozwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia Mtandao wa Wanawake na Katiba, Uchaguzi na Uongozi unaoratibiwa na Mfuko wa Ufadhili wa Wanawake Tanzania (WFT_T) pamoja na Mitandao mingine ya Tapo la Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi",amesema Prof. Ruth.
Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena ambaye ni Mwanachama wa TGNP akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025).

Ameeleza kuwa, Walengwa wa kwanza wa Ilani hiyo ni Wanawake ambao ni wapiga kura, wenye nia na haki ya kushiriki katika uchaguzi na hatimaye kushiriki katika kuliongoza taifa kwenye maeneo mbalimbali.

"Ilani hii ni wito kwetu sisi wanawake wote kuungana na kupaza sauti kwa pamoja tukiwa na ajenda moja ya kudai mabadiliko ya mfumo/mifumo kandamizi na yenye kutubagua. Kwa pamoja tunasema hatuwezi kujenga demokrasia thabiti kama chaguzi zetu si huru na za haki kwa mtazamo wa jinsia",ameongeza.

"Ilani hii pia inailenga serikali iliyoko madarakani, tukiitaka serikali , taasisi na vyombo vyote vinavyohusika na uchaguzi viwajibike kuzingatia mikataba, itifaki, matamko ya kimataifa na kikanda pamoja na misingi ya kikatiba iliyoainishwa kwenye dira ya taifa ya 2025. Ilani inatoa wito kwa serikali kuchukua hatua za maksudi za kusawazisha mazingira ya uchaguzi ili wanawake waweze kushiriki bila vikwazo vinavyowabagua", amesema Prof. Ruth.

Walengwa wengine ni vyama vya siasa ambavyo katika muktadha wa uchaguzi vina uwezo mkubwa wa kuamua ni nani aingie kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi, ni nani afungiwe milango na ni nani aungwe mkono hadi hatua za ushindi.

Vilevile Ilani hiyo inalenga vyombo vya habari, kutokana na nguvu ya vyombo hivi kuleta mabadiliko ya mtazamo kuhusu nafasi ya mwanamke katika uongozi na taifa lakini pia walengwa wengine ni wapiga kura wote na hasa wanawake kutokubali kununuliwa au kudanganywa kuuza kura zao kwa wenye uchu wa madaraka.
Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena ambaye ni Mwanachama wa TGNP akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) leo Ijumaa Novemba 10,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena ambaye ni Mwanachama wa TGNP akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) 
Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena (katikati kushoto) ambaye ni Mwanachama wa TGNP  akikata utepe ishara ya uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) 

Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena (katikati) ambaye ni Mwanachama wa TGNP akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) 
Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena ambaye ni Mwanachama wa TGNP akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025)
Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena (katikati) ambaye ni Mwanachama wa TGNP akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025)
Mwanaharakati Mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena (katikati) ambaye ni Mwanachama wa TGNP akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025)

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com