Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake Novemba 25, Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na Taasisi inayoshughulika na haki za wanawake VIKES imefanya mkutano wa Kuimarisha Usawa wa Kijinsia na Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo wenye kauli mbiu "Kujenga Daraja: Mkutano wa Usawa wa Kijinsia na Uhuru wa Habari", leo Novemba 24,2023 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa MISA TAN Bi. Elizabeth Riziki amesema mkutano huo unalenga kuleta pamoja wahusika wa serikali, wataalamu wa vyombo vya habari, na wawakilishi kutoka taasisi za kijamii ili kuimarisha ushirikiano, kubadilishana mawazo, na kutafuta mikakati itakayochangia kukuza usawa wa kijinsia na uhuru wa vyombo vya habari.
“Malengo ya mkutano huu uliokutanisha Asasi za Kiraia, Waandishi wa Habari, Serikali na wadau wa maendeleo ni kuweka jukwaa la kuwaleta pamoja wahusika wa serikali, wataalamu wa vyombo vya habari, na wawakilishi wa taasisi za kijamii kujenga uhusiano, kubadilishana mawazo na kuchunguza ushirikiano unaowezekana”,amesema.
“Lengo jingine ni Kujiandaa kwa Siku 16 za Uanaharakati kwa kuunganisha nguvu katika kampeni kubwa ya kimataifa ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Dhuluma za Kijinsia, kuunda msukumo kwa juhudi endelevu zaidi baada ya tukio la siku moja”,ameeleza Elizabeth.
Malengo mengine ni kukuza Usawa wa Kijinsia kwa kushirikisha washiriki katika mazungumzo, na mawasilisho yanayobainisha jukumu la vyombo vya habari katika kukuza usawa wa kijinsia na kupambana na dhuluma dhidi ya wanawake. Kuhamasisha maendeleo ya ripoti na simulizi zinazozingatia masuala ya kijinsia.
“Lengo jingine ni Kukuza Uhuru wa Habari kwa Kusisitiza umuhimu wa vyombo vya habari huru na visivyopendelea katika jamii ya kidemokrasia. Kujadili changamoto zinazokabiliwa na wataalamu wa vyombo vya habari na kuchunguza njia za kulinda na kukuza uhuru wa habari”,amesema.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN), Bi. Elizabeth Riziki akizungumza wakati akifungua mkutano huo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN), Bi. Elizabeth Riziki akizungumza wakati akifungua mkutano huo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN), Bi. Elizabeth Riziki akizungumza wakati akifungua mkutano huo
Social Plugin