Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA MAJI MHANDISI MAHUNDI ASHIRIKI MKUTANO WA AFRIKA KUHUSU USAWA WA KIJINSIA

Tanzania imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa ngazi ya juu wa Afrika kuhusu ufadhili wa usawa wa kijinsia uliofanyika Jijini Dar es Salaam uliolenga kujadili namna ya kukuza haki za wanawake kiuchumi  na usawa wa Kijinsia.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na mawaziri wa fedha na Jinsia Afrika umedhamiria  kushughulikia kwa utaratibu matokeo ya uchumi na kuchochea kujitolea zaidi kwa ufadhili wa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Katika Mkutano huu  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi   Dk.Hussein Ali Mwinyi ndiye mgeni rasmi pia mawaziri na Viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwamo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akimuwakilisha Waziri wa Maji Mheshimiwa Juma Aweso( Mb).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com