*****
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini ameutolea ufafanuzi ujenzi wa kituo cha polisi kilichopo wilayani Butiama mkoani Mara kilicholeta taharuki kwa wananchi baada ya kudaiwa kujengwa kwa shilingi Milioni 802.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya kutembelea mikoa minne ambayo ni Mara ,Mwanza,Simiyu na Geita kwa lengo la kutembelea na kukagua miradi yote inayotekelezwa na vyombo vilivyopo chini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa miradi ya ujenzi kwa polisi, magereza, uhamiaji, zimamoto na uokoaji sambamba na kuzungumza na wafungwa na mahabusu katika magereza ya mikoa yote aliyopita
kwenye vituo vya polisi na magereza .
Anaeleza kuwa mpaka sasa jengo hilo ambalo ujenzi wake bado haujakamilika linagharimu shilingi Milioni 366 na serikali imetoa Milioni 500 ambapo makadirio ya gharama za ujenzi yakiwa ni Milioni 802 na kwamba siyo ujenzi umeshatumia fedha zinazosambaa kwenye mitandao na wananchi wakihoji ukubwa wa gharama hiyo ikilinganishwa na jengo linalojengwa.
"Kutokana na sintofahamu hiyo, niliwasiliana na Waziri tukakubaliana Katibu Mkuu (Kaspar Mmuya) aunde kamati ya uchunguzi wa jambo ilo timu imeundwa na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa ndani kamati inayojumuisha wataalamu wa manunuzi, wataalamu wa ukadiriaji wa majenzi, wahandisi na wakaguzi ili kufanya uchunguzi kuanzia ngazi ya ukadiriaji wa gharama za ujenzi hadi hatua ujenzi ulipofikia kama kutabainika kuna upungufu au uongezaji wa gharama usio na haki wahusika lazima wachukuliwe hatua stahiki" ,anaeleza Sagini.
Anaeleza kuwa timu iliyoundwa haifungamani na upande wa jeshi hilo wala wizara yake hivyo ifuatilie kwa kina na kujiridhisha na taarifa hiyo itawasaidia kufanya maamuzi sahihi pia wataalamu wanaojenga kituo hicho ni jeshi la polisi ikithibitika kuna watu ama mtu mwenye nia ovu watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa imma na kisheria.
Hivyo aliwaomba wananchi wananchi na watanzania kwa ujumla wawe na subira na chombo hicho kilichoundwa kwani baada ya uchunguzi kukamilika picha halisi ya ujenzi huo unaotarajia kukamilika Desemba mwaka huu utaonekana hasa .
Social Plugin