Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU 'NBS' YATOA MAFUNZO YA USAMBAZAJI NA MATUMIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 KWA VIONGOZI NA MAKUNDI MBALIMBALI MANISPAA YA SHINYANGA

Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akimkabidhi Ramani ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kuwajengea uwezo wa kutafsiri, kuchambua na kuyatumia matokeo ya Sensa katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa sera na mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo Jumanne Novemba 28,2023 , Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesema mafunzo hayo yatawaongeza uelewa na ujuzi wa kutumia matokeo ya Sensa katika kufanya maamuzi yenye tija ya maendeleo ya wananchi.

"Naipongeza NBS kwa kazi kubwa wanayoendelea kufanya ya kusimamia kwa weledi utekelezaji wa shughuli za Sensa kwa mafanikio makubwa. Uwepo wenu hapa leo unadhihirisha mnavyotekeleza kwa vitendo dhamira za kweli za Serikali zetu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Viongozi wetu hawa, wameelekeza matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yawafikie wadau wote na yatumike kikamilifu ili kuchagiza na kuharakisha maendeleo ya nchi yetu",amesema Mhe. Samizi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

"Kwa kuwa suala la kupanga mipango ya maendeleo ni shirikishi na linaanzia ngazi za chini hadi Taifa; sisi tunao wajibu wa kuratibu suala zima la upangaji wa mipango na programu za maendeleo kuanzia Mtaa au Kijiji, kata, halmashauri, wilaya na mkoa. 

Hivyo mafunzo haya yanatuongezea ujuzi na kupata uzoefu zaidi kutoka kwa wataalamu wetu namna bora ya kutumia matokeo ya Sensa katika kutekeleza majukumu yetu",ameeleza Mhe. Samizi.

Amefafanua kuwa, Matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa yatawezesha kuongezeka kwa ufanisi katika matumizi ya rasilimali za nchi kwa kuzingatia mahitaji halisi na mazingira wanamoishi wananchi. 

"Mafunzo haya yatatuwezesha pia kuhakikisha mipango yetu inakuwa jumuishi kama ujumbe wa kaulimbiu ya Sensa wa awamu hii ya Tatu inavyosema “Matokeo ya Sensa ya Sita, Mipango Jumuishi kwa Maendeleo Endelevu, ameongeza.

Amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia pia watakuwa na mipango itakayotoa majibu ya changamoto mbalimbali za maendeleo zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Shinyanga hususan mipango inayojielekeza katika kuondoa umaskini wa kipato na usio wa kipato na hatimae kuinua kiwango cha hali ya maisha kama inavyoelekeza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020.
Mafunzo yakiendelea

Amebainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekamilisha na kuzindua ripoti mbalimbali za Sensa ambapo Ripoti hizo zimebainisha hali ilivyo katika sekta mbalimbali kuanzia ngazi ya Taifa, mkoa, wilaya na nyingine hadi ngazi ya kata.

"Matumizi ya matokeo haya ya Sensa yanatusaidia kufahamu tuko wangapi katika maeneo yetu kwa jinsi, umri, fursa za kiuchumi zilizopo pamoja taarifa nyingine za kidemografia, kiuchumi na mazingira. 

Matokeo ya Sensa yanabainisha hali halisi ya upatikanaji na ubora wa huduma za kijamii kama vile huduma za maji, miundombinu ya barabara, huduma za afya, elimu, nishati, masoko, mabenki na mawasiliano. Hivyo, matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ni nyenzo muhimu ya kisera katika kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi. Hatuna budi kuyaelewa na kufahamu matumizi yake kwani ni jambo la msingi ambalo litachochea kasi ya kutatua kero za wananchi katika mkoa wetu", ameeleza.

Amewasisitiza viongozi na watendaji wote kuwa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na takwimu nyingine za kisekta zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ziwe ndio msingi wa kufanya maamuzi ya maendeleo katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo.

Amesema wananchi wana matumaini kuwa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yatawezesha kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao ya kila siku.

"Matumaini hayo yamejengwa na wito wa viongozi wetu wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye wakati wote wa utekelezaji wa Sensa hadi kuzinduliwa kwa matokeo ya mwanzo ya Sensa mwezi Oktoba Mwaka 2022 amekuwa akisisitiza umuhimu wa matumizi ya matokeo ya Sensa. Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Rais alisisitiza kuwa, matokeo ya Sensa yanakwenda kuleta mabadiliko katika mwenendo wetu wa kufanya maamuzi, uandaaji wa sera, mipango, ufuatiliaji na ufanyaji tathmini ya utekelezaji wa sera na mipango yetu ya maendeleo",amesema.

"Hivyo, tunayo dhima kubwa ya kukidhi matarajio hayo ya wananchi wetu na pia kuhakikisha tunakwenda bega kwa bega na dhamira ya Rais wetu kwa kukakikisha tunatekeleza kikamilifu Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022",amesema Mhe. Samizi.
Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ameshauri Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa Makundi mbalimbali katika jamii pindi wanapohitaji takwimu kwenye maeneo yao waombe taarifa kwenye ofisi za NBS.

"Tunajua mna mahitaji mengi kwenye maeneo yenu kutokana na matokeo haya ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, tunaomba kama kuna mnahitaji ya takwimu, tuandikieni barua kwenye ofisi za NBS, tutawapatia takwimu mnazohitaji kulingana na eneo unalohitaji",amesema Mugambi.

 Akitoa Wasilisho la Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary amesema mkoa wa Shinyanga una wakazi 2,241,299 ambapo halmashauri yenye watu wengi ni Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (watu 468,611) ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ( watu 453,654) na halmashauri yenye  idadi ndogo ya watu katika mkoa wa Shinyanga ni Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (watu 214, 744).

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 28,2023 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga 

Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anold Mkombe  akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary akitoa Wasilisho la Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary akitoa Wasilisho la Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022

Mrasimu Ramani kutoka 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Nolasco John akitoa wasilisho la matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 kwa njia ya ramani
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea

Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedict Mugambi ambaye ni Meneja Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akimkabidhi Ramani ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia).
Madiwani wakiteta jambo wakati wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa, Wilaya na Wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii kwa Manispaa ya Shinyanga

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com