Picha : MAADHIMISHO SIKU YA SHUKRANI KWA MLIPAKODI SHINYANGA YAFANYIKA… KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRIT LTD YANG’ARA TUZO YA MCHANGIAJI MKUBWA WA KODI

Matembezi ya hisani na walipakodi, watumishi wa TRA pamoja na wanafunzi wa Klabu za Kodi kutoka shule na vyuo mbalimbali.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga imeadhimisha Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi ikiongozwa na kauli mbiu ‘Kodi yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike’ huku ikijivunia kukusanya shilingi Bilioni 32.8 (32,878,016,785.23/= sawa na ufanisi wa asilimia 83.21 ya lengo la kukusanya shilingi Bilioni 39.5 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi yamefanyika leo Alhamisi Novemba 30,2023 katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga yakitanguliwa na matembezi ya hisani ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Makamu Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bi. Anna Mndeme amesema lengo la maadhimisho ya Wiki ya Shukrani kwa mlipakodi ni kuwatambua na kuwashukuru walipakodi wote kwa mchango wao katika taifa bila kujali ukubwa au udogo wao.

“Katika wiki hii tumetoa elimu ya mlipakodi, kutoa misaada mbalimbali kama vile Tanki la kuhifadhia maji katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu na chakula kwenye makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto na kuwatunuku vyeti na zawadi walipakodi na wadau wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mchango mkubwa zaidi katika kusaidia na kuwezesha shughuli za usimamizi wa kodi”,ameeleza.
Makamu Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bi. Anna Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga

“Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 TRA Mkoa wa Shinyanga ina lengo la kukusanya shilingi Bilioni 12.5 na tumeuanza mwaka kwa mafanikio ya kuridhisha kwani katika robo ya kwanza (Julai – Septemba 2023), tumefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 3.1 sawa na ufanisi wa asilimia 123.05 ya lengo la kukusanya shilingi 3,066,100,000/=”,amesema Mndeme.

Aidha ametoa rai kwa walipakodi kuendelea na kuongeza uhiari na utayari katika kutimiza wajibu wao kisheria kujisajili kama walipakodi kwa wale ambao bado hawajasajiliwa, kuwasilisha ritani za kodi kwa usahihi pamoja na kulipa kodi kwa wakati ili kujenga taifa linalojitegemea.

Hata hivyo Mndeme amesema bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutotumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) hivyo akatoa wito kwa kila mmoja kuwajibika kwa kutoa risiti sahihi ya EFD anapouza au kudai risiti sahihi ya EFD anaponunua bidhaa za huduma mahali popote nchini.

Katika hatua nyingine amesema TRA itaendeleza jitihada za utatuzi wa migogoro na mashauri ya kodi nje ya mahakama kwa njia ya maridhiano ya kisheria ili kuimarisha Imani ya walipakodi na kutoa muda wa kutosha kujikita katika shughuli za kibiashara badala ya kuendesha mashauri ya kodi.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga

Kwa upande wake, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameipongeza TRA Mkoa wa Shinyanga kwa mwenendo mzuri wa makusanyo ya kodi hali inayoonesha ni kwa kiasi gani wanajituma katika kutekeleza majukumu yao ya kukusanya kodi lakini pia inaonesha jinsi gani walipa kodi wanatekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari ili kuiletea nchi maendeleo.

Mhita ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara kutumia mashine za EFD ipasavyo badala ya kutoa kiwango pungufu kuliko kiwango cha pesa walichotoa kupata huduma au kununua bidhaa huku akiwataka wale wenye sifa za kununua au kutumia mashine za EFD wanunue na kuzitumia.

“Ili kupanua wigo wa kukusanya kodi na kuongeza mapato ya serikali, natoa wito kwa kila mwananchi atimize wajibu wake; wafanyabiashara watoe risiti na wanunuzi wadai risiti, walengwa kununua mashine za EFD na kujisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) pamoja na leseni ya biashara”,amesema Mhita.
Mcheza ngoma za asili akicheza na nyoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi

“Pia wananchi watoe taarifa za wakwepa kodi kwa TRA, kuacha kushiriki biashara yoyote ya magendo, kutoa taarifa ya mabadiliko ya biashara kwa TRA,kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati, kujenga desturi ya kuwasiliana kwa karibu na TRA kwa mfanyabiashara mmoja mmoja ili kutatua changamoto zinapojitokeza na kuwasilisha ritani za kodi kwa wakati “,ameongeza Mhita.

Maadhimisho ya Siku ya Mlipakodi Mkoani Shinyanga yametanguliwa na Matembezi ya hisani na walipakodi, watumishi wa TRA pamoja na wanafunzi wa Klabu za Kodi kutoka shule na vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga.

Katika maadhimisho hayo ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi, TRA imetoa tuzo kwa walipakodi walioweza kuichangia serikali kiasi kikubwa zaidi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo Kampuni ya East African Spirit limited imetangazwa kuwa mchangiaji mkubwa wa kodi mkoani Shinyanga na kwa upande wa walipa kodi wakubwa (Large Taxpayers) pia Kampuni ya East African Spirit Limited imeibuka mshindi wa kwanza ikifuatiwa na Sakisa & CO Limited.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, meza kuu wakipiga picha na walipakodi waliopata tuzo na zawadi

Aidha Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamonds Limited umepata tuzo ya Walipakodi wakubwa katika mikoa iliyo chini ya Idara kubwa ya walipakodi.
 
Upande wa walipakodi wa kati (Medium Taxpayers mshindi wa kwanza ni Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd akifuatiwa na Leonard Kasoni Manaha na I DROP (T) Limited wakati Walipakodi wadogo (small taxpayers) mshindi wa kwanza ni Ally Nassor Rashid akifuatiwa na Ally Hamad Hilal na Benno Damian Urassa.

Aidha kwa upande wa washindi ngazi ya wilaya washindi ni A.A Gimbi Company Limited akifuatiwa na Nkamba Company (T) Limited na African Buffalo Safari Trackers Limited.

Pia TRA imezitangaza taasisi zenye ushirikiano bora TRA kwa mwaka 2022/2023 ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Ofisi ya Usalama wa Taifa, Benki ya CRDB pamoja na kituo cha matangazo Redio Faraja Fm Stereo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Novemba 30,2023 katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Novemba 30,2023 katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga.
Makamu Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bi. Anna Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Makamu Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bi. Anna Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Mdessa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Mdessa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa TCCA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Kifunda Manyama akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Walipa kodi mkoa wa Shinyanga wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Mdessa (kushoto) na Mwenyekiti wa TCCA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Kifunda Manyama wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi  (kushoto) Makamu Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bi. Anna Mndeme wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Wananchi wakifuatilia matukio kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Wananchi wakifuatilia matukio kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Burudani ikiendelea kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Mcheza ngoma za asili akicheza na nyoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Mcheza ngoma za asili akicheza na nyoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi

Mcheza ngoma za asili akicheza na nyoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Mfanyakazi wa TRA Salum akishika nyoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Vijana wakionesha umahiri wa kucheza muziki kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Walimu wakitoa burudani kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Walimu wakitoa burudani kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo kwa walipakodi walioweza kuichangia serikali kiasi kikubwa zaidi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo Kampuni ya East African Spirit limited imetangazwa kuwa mchangiaji mkubwa wa kodi mkoani Shinyanga na kwa upande wa walipa kodi wakubwa (Large Taxpayers) pia Kampuni ya East African Spirit Limited imeibuka mshindi wa kwanza. Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Gladness Gasper Kileo akipokea tuzo
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidh tuzo kwa walipakodi walioweza kuichangia serikali kiasi kikubwa zaidi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akipokea tuzo/zawadi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akikabidhi tuzo/zawadi kwa walipakodi 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, meza kuu wakipiga picha na walipakodi waliopata tuzo na zawadi

Wafanyakazi wa TRA wakipiga picha ya pamoja kabla Matembezi ya hisani na walipakodi, watumishi wa TRA pamoja na wanafunzi wa Klabu za Kodi kutoka shule na vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga kutoka ofisi za TRA Mkoa wa Shinyanga hadi Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga

Makamu Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bi. Anna Mndeme (katikati), Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Mdessa (kushoto) na Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi  wakiongoza Matembezi ya hisani na walipakodi, watumishi wa TRA pamoja na wanafunzi wa Klabu za Kodi kutoka shule na vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga kutoka ofisi za TRA Mkoa wa Shinyanga hadi Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga
Matembezi ya hisani na walipakodi, watumishi wa TRA pamoja na wanafunzi wa Klabu za Kodi kutoka shule na vyuo mbalimbali yakiendelea

Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi yakiendelea
Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi yakiendelea
Wananchi wakifuatilia matukio kwenye maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi
Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi yakiendelea
Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi yakiendelea
Picha za kumbukumbu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Shinyanga

Picha za kumbukumbu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post