Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu na chakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi inayoongozwa na kauli mbiu ‘Kodi Yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike’.
Misaada hiyo imekabidhiwa leo Jumatano Novemba 29,2023 na Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi akiwa ameambatana na Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Tanki la kuhifadhia maji katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Mossi amesema TRA imetoa tanki hilo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa walipa kodi ili kupunguza changamoto ya vifaa vya kutunzia maji katika hospitali hiyo hususani katika Wodi ya Wazazi na kufulia.
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi (kushoto) akizungumza wakati akikabidhi Tanki la kuhifadhia maji katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
“Sisi TRA kila mwaka huwa tuna taratibu wa kurudisha shukrani kwa Walipa kodi kwa hiyo tunatenga wiki moja kwa mwaka kwa ajili ya kutoa shukrani kwa walipa kodi ambapo hiyo wiki inaambatana na elimu kwa walipa kodi , kutoa misaada mbalimbali na kutoa tuzo kwa wafanyabiashara waliolipa kodi vizuri kwa mwaka husika”,amesema.
“Tumekuja Kishapu kwa ajili ya kutoa msaada wa Tanki moja la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000/=. Tumetoa Tanki hili la kuhifadhia maji ili wagonjwa wanapokuja hapa waone kwamba hata wanapolipa kodi inarudi kuja kufanya maendeleo na kutoa huduma. Wanapoona hivyo waone umuhimu wa kulipa kodi”,ameeleza Mossi.
Katika hatua nyingine amehawamasisha wananchi kulipa kodi huku akisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutoa risiti na wanunuzi wa bidhaa kudai risiti.
“Kwa TRA tuna Kampeni ya Tuwajibike ambayo inawagusa watu wote wakiwemo wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa. Mfanyabiashara anapouza anatakiwa ahakikishe anatoa risiti na mtumiaji wa huduma na bidhaa anatakiwa adai risiti ili serikali ipate mapato ambayo yanafanya shughuli zote za maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, barabara, huduma za elimu n.k”,amesema.
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi (aliyevaa koti jeusi) na Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi ( wa kwanza kushoto) wakikabidhi vyakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Akiwa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto ambayo sasa yana wahudumiwa 20, Mosi amesema wametoa msaada wa chakula ikiwemo mchele, sukari, unga na mafuta ya kupikia ili kutoa fadhila kwa jamii kwani kundi hilo la wazee ni muhimu halipaswi kusahaulika.
Akizungumza wakati wa kupokea Tanki la Maji, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala amesema tanki hilo la kuhifadhia maji litasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu.
“Hii inatukumbusha wananchi kuona umuhimu wa kulipa kodi bila shuruti, kile tunachotoa kinarudi kwa wananchi kusaidia kushughuli za maendeleo”,amesema Swalala.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Dkt. Mohamed Mkumbwa ameishukuru TRA kuwapatia tanki hilo la maji ambalo amesema litasaidia kupunguza adha ya upatikanaji wa maji hasa katika wodi ya Wazazi ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu wanawake wajawazito zaidi ya 450 wanafika kujifungua katika hospitali hiyo.
Naye, Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Bi. Sophia Kang’ombe ameishukuru TRA kwa kuwapatia msaada chakula wazee huku akitaja baadhi ya changamoto zilizopo hapo kuwa ni upungufu wa vyumba ambapo wazee wanalazimika kulala wawili ndani ya chumba kimoja na ukosefu wa uzio kwenye makazi hayo.
Nao baadhi ya wazee akiwemo Katarina Maige na Juakali Mihangwa wameishukuru TRA kwa kuwapatia msaada huo na kuomba wadau mbalimbali wafike kwenye makazi hayo ili kutatua changamoto zinazowakabili.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi (kushoto) akizungumza wakati akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala ,Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu leo Jumatano Novemba 29,2023 katika hospitali hiyo iliyopo katika kata ya Kishapu Wilayani Kishapu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi (kushoto) akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala ,Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
Wafanyakazi wa TRA Shinyanga na viongozi mbalimbali wakipiga picha wakati TRA ikikabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu

Wafanyakazi wa TRA Shinyanga wakipiga picha wakati TRA baada ya kukabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi akizungumza wakati akikabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Dkt. Mohamed Mkumbwa akiishukuru TRA kuwapatia Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Dkt. Mohamed Mkumbwa akiishukuru TRA kuwapatia Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali hiyo.
Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi (katikati) akiongoza kutamka kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi inayosema ‘Kodi Yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike’.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akizungumza wakati TRA ikikabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
Diwani wa kata ya Kishapu Mhe. Joel Ndeto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu akizungumza wakati TRA ikikabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fadhili Joseph Mvanga akizungumza wakati TRA ikikabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
Katibu wa CCM kata ya Kishapu, Colnel Zengo akizungumza wakati TRA ikikabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
Mmoja wa wananchi waliokuwa wanapatiwa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu akizungumza wakati TRA ikikabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika hospitali.Muonekano wa sehemu ya chakula kilichotolewa na TRA Mkoa wa Shinyanga katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mkoani Shinyanga
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi akizungumza wakati akikabidhi chakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga

Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akizungumza wakati TRA ikikabidhi vyakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga

Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi (aliyevaa koti jeusi) na Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi (wa kwanza kushoto) wakikabidhi vyakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga
Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi (aliyevaa koti jeusi) na Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi ( wa kwanza kushoto) wakikabidhi vyakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga
Mzee Juakali Mihangwa akitoa neno la shukrani wakati TRA Mkoa wa Shinyanga ikikabidhi chakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga
Mzee Juakali Mihangwa akimpa mkono wa shukrani Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga Estomih Mossi wakati TRA ikikabidhi chakula chakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto
Bi. Katarina Maige Juakali akitoa neno la shukrani wakati TRA Mkoa wa Shinyanga ikikabidhi chakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Bi. Sophia Kang’ombe akitoa neno la shukrani wakati TRA Mkoa wa Shinyanga ikikabidhi chakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu na wazee katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin