Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Afisa Uchunguzi Mwandamizi TAKUKURU mkoa wa Tanga Frank Mapunda ameeleza mikakati na mafanikio yaliyopata kwa miezi mitatu kwa kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa miradi ya BOOST.
Mapunda amesema kuwa vikao vilivyofanyika mwanzoni mwa miradi Boost vimesaidia kuziba mianya ya rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Tanga.
Katika utekelezaji wa majukumu ya uzuiaji na kupambana Rushwa Mapunda amesema Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga imefanikiwa kufanya uchambuzi wa mifumo Tisa (9) ili kuleta tija na mifumo imara isiyokwamisha utoaji wa huduma Bora kwa wananchi .
Aidha Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau imepokea taarifa 142 ambapo taarifa 89 ni vitendo vya Rushwa na taarifa 53 si za vitendo vya rushwa na mashauri saba (7) mapya yamefunguliwa mashtaka Hadi Sasa Jamuhuri imeshinda shauri 1 na 26 yanaendelea mahakamani.
Social Plugin