Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MIAKA 30 YA TGNP: VIJANA WATAKIWA KUFUATA NYAYO ZA WANAHARAKATI WAKONGWE, KULETA MABADILIKO


Mwanaharati mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena, akizungumza wakati wa mdahalo wa kuangalia, safari ya Harakati, Nyayo zetu, urithi wetu wakati wa Tamasha la Jinsia la 15, na miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanaharati mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena, akizungumza wakati wa mdahalo wa kuangalia, safari ya Harakati, Nyayo zetu, urithi wetu wakati wa Tamasha la Jinsia la 15, na miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam. 

Na Deogratius Temba - Dar es salaam

VIJANA wametakiwa kuweka mikakati ya kufuata nyayo za wanaharakati wakongwe walioanzisha majukwaa ya Utetezi wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia nchini tangu maika ya 1990 ili kuchangia uwepo wa mabadiliko chanya ya kishera,kisheria na kimfumo. 

Hayo yamesemwa  leo Novemba 8,2023 na Mwanaharati mkongwe wa Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia, Profesa Ruth Meena, wakati wa mdahalo wa kuangalia, safari ya Harakati, Nyayo zetu, urithi wetu wakati wa Tamasha la Jinsia la 15, na miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam. 

“Tamasha hili ni ushuhuda, tunao waacha msiache hii kitu wazee wenu tumepigana sana, harakati hizi zinahitaji ujenzi wa nguvu ya pamoja. Nguvu ya shirika moja haiwezi kubomoa mifumo kandamizi. Tapo halina mfumo mmoja wa kuliunda, tunagawana kutokana na uwezo wa shirika kitaaluma, ili tufanikiwe tuligawana maeneo ya kufanyia kazi. Mfano masuala ya Habari walifanya Tamwa, sheria walifanya Tawla na Wilac ,  TAPO hili limesambaa vizuri, kuna majukwaa, makubwa na imara ambayo tumeshajenga, tumeweka misingi, tunaomba vijana muendeleze kuanzia hapa”, amesema prof. Ruth na kuongeza

Tunajivunia kwamba tuliweza kujenga mahusiano na serikali, mdau muhimu katika kubadilisha mifumo ya kisera na kisheria ni serikali, huwezi kupiga kelele huko nje pekee yako ukategemea mabadiliko, ni lazima kuanza kwa kujenga mahusiano na kuwaeleza maana ya jambo unalolihitaji, na madhara yake na faida ya mabadiliko unayoyahitaji…” 

Aidha Profesa Ruth amebainisha kwamba katika harakati hizo, kuna changamoto zilizojitokeza ambazo ni pamoja na upinzani mkubwa wa kupinga marakebisho ya baadhi ya sera na sheria ili ziwe na mtazamo wa kijinsia kwa kigezo kwamba zinaenda kuwanufaisha Zaidi wanawake. 

Lakini pia ameeleza kuwa, jamii ya kitanzania bado ina mtazamo hasi kuhusu masuala ya usawa wa Kijinsia na haki za wanawake, mila na desturi kandamizi zinachangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.

 TAZAMA VIDEO PROF. RUTH MEENA AKIZUNGUMZA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com