Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Amend wametoa tuzo kwa wanafunzi ambao wameibuka washindi wa michoro ya usalama barabarani kupitia kampeni ya Be Road Safe kwa njia ya sanaa.
Katika utoaji wa tuzo huo umefanyika katika Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ambaye aliwakilishwa ba Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo .
Kampeni hiyo inalenga kuleta mageuzi ya usalama wa watoto na vijana barabarani nchini Tanzania huku ikielezwa wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Kubugumo, Kufaru, Msewe, Kibasila na Mtambani wameshiriki katika kampeni hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo shindano la kuchora.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, wakati wa utoaji tuzo hizo kwa washindi, Mkuu wa Wilaya Halima Bulembo amesema wanaipongeza kampuni ya Puma Energy Tanzania pamoja na Ammend kwa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watoto walioko shule za msingi.
Asema mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto walioko katika shule za msingi yatasaidia kupunguza ajali za barabarani hususan katika maeneo ambayo mafunzo hayo yametolewa huku akishauri elimu hiyo yatolewe nchi nzima kuongeza uelewa.
Amesisitiza Serikali inaamini kwa kufanya hivyo kitaokolewa kizazi cha sasa na kijqacho kwa kuwa elimu ya matumizi bora ya barabara inaendelea kusambaa.
Amesema kuwa kupitia mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hususan walioko katika shule za msingi Puma imefanya jambo kubwa katika kuepusha ajali za barabarani ambazo zimekuwa sikiisababishia nchi hasara kubwa kwa kupoteza nguvu kazi na mali.
"Mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yaliyotolewa na Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na Ammend katika shule tano ni vyema yakatolewa pia katika shule nyingi zaidi kuwajengea uwelewa watoto wangi wa Dar es Salaam na hata nje ya mkoa huo.
"Serikali ya mkoa (Dar es Salaam) tunaamini kuwa kwa kufanya hivi tunaokoa kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa elimu ya matumizi bora na sahihi ya barabarani inaendelea kusambaa," amesema Bulembo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, amesema mafunzo yaliyotolewa kwa wanafunzi hao ni utekelezaji wa mpango wa 'Be road safe Africa) unaotekelezwa na Ammend katika nchi tano za Afrika ambazo ni Zambia, Zimbabwe, Tanzania, Botswana na Ghana.
Amesema kuwanzishwa kwa mpango huo kunatokana na takwimu mbaya za ajali za barabarani ambazo zinasababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.
"Nchini Tanzania pekee Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani kimetoa takwimu zinazoonyesha kutokea kwa vifo 1,545 na majeruhi 2,278 kwa mwaka 20222 kutokana na ajali 1,720 za barabarani.
Fatma akizungumzia kampeni hiyo ya 'Be Road Safe' amesema kuwa ni jukwaa muhimu shirikishi linalokuza jamii salama kwa watoto.
"Kupitia mashindano hayo ya kuchora tumeongeza ubunifu na uelewa thabiti wa kanuni za usalama barabarani miongoni mwa wanafunzi na kuongeza ufahamu kwa jamii ya Watanzania.
Amesema tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 2013 'Be Road Safe' umekuwa mwanga wa matumaini na kwamba ni msingi wa kimkakati wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) wa kampuni hiyo chini ya mpango mkuu wa 'Be Puma Safe' ambao pia unajumuisha uwezeshaji wa wananchi hususan vijana.
Hafla hiyo iliyofanyika Shule ya Msingi Kibugumo ilihidhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Michael Deleli, Mkurugenzi wa Shirika la Ammend Simon Kalolo, walimu na wanafunzi kutoka shule zilizoshiriki mafunzo na shindano hilo.
Mwanafunzi wa darasa sita katika Shule ya Msingi Kibugumo Feisali Msiakwe akinyanyua juu kikombe cha ushindi baada ya mchoro wake wa kuelimisha kuhusu usalama barabarani kushinda katika shindano la michoro ya usalama barabarani kwa Mkoa wa Dar es Salaam.Feisali amepata kitita cha Sh.500, 000 na shule yake baada ya kuibuka mshindi wa mchoro wa usalama barabarani na kuifanya shule yake imepata Sh.milioni tano ambazo zimetolewa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kupitia Mkurugenzi wake Fatma Abdallah(wa kwanza kushoto waliosimama.)
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo(wa tatu kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Abdallah( wa kwanza kushoto) wakiwa wameshika mfano wa hundi ya Sh.milioni tano iliyotolewa kwa Shule ya Msingi Kibugumo baada ya mwanafunzi wake Feisali Msiakwe ( wa nne kushoto) kuibuka mshindi wa mashindano ya mchoro wa usalama barabarani katika mkoa wa Dar es Salaam.Mashindano hayo yameandaliwa na Puma kwa kushirikiana na Shirika la Amend Tanzania.Wengine katika picha hiyo ni walimu na wadau wa usalama barabarani.
Social Plugin