Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 3.4 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara, elimu, miradi ya maendeleo, afya na vifaa tiba katika halmashauri ya wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel alipo mwakilishwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba katika kilele cha Harambee na Ibada ya kuadhimisha miaka saba ya Dayosisi ya KKKT Mwanga
Dkt. Mollel amesema kuwa katika fedha hizo zilizotolewa halmashauri hiyo itanufaika kwa kupatiwa Hospitali ya Wilaya itakayosaidia kutoa Huduma za afya kwa wakazi wa mwanga na maeneo jirani.
Vile vile amesema kuwa imesaidia kuongeza vifaa tiba, dawa pamoja na vitendanishi ili kuhakikisha wananchi wa halmashauri hiyo wanapata Huduma za afya kwa usahihi na wakati
“Nitoe wito kwenu kuendelea kumuombe Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutuongoza vyema na kutuletea maendeleo wanamwanga na Taifa kwa ujumla”, amesisitiza Dkt. Mollel