Mvua
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kuanzia leo Jumatano Novemba 22 hadi Novemba 25 ambazo huenda zikasababisha mafuriko kwa maeneo machache ambayo yanaweza kusababisha vifo.
Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Kupitia taarifa ya Mamlaka iliyotolewa jana Jumanne Novemba 21, 2023, imetaja athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya barabara kutopitika kutokana na mafuriko pamoja na vifo kwa siku hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.
Via EATV
Social Plugin