Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTATURU: RAIS SAMIA AMEIMARISHA AFYA IKUNGI




MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki tukio la kihistoria la kupokea vifaa vya afya katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 73.

Vifaa hivyo ni Jenereta,meza ya kufanyia upasuaji,mashine ya Ultra Sound ,kifaa cha joto kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na mashine ya kunyonya uchafu kutoka mwilini.

Akizungumza Novemba 20,2023,Mtaturu amesema hiyo ni hatua kubwa katika kufikia utoaji wa huduma bora za afya.

“Hii inafuatia baada ya kukamilisha majengo ya hospitali ya wilaya na sasa serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD),wanakamilisha uletaji wa vifaa tiba ili kuwa tayari kutoa huduma zote hapa Ikungi ikiwemo huduma ya upasuaji,

“Kwa niaba ya wananchi wa Singida Mashariki tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha za miradi na hivyo kutekeleza kwa vitendo sera ya uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi,”.amesema.

Meneja wa Bohari ya Dawa Mwanashehe Jumaa akikabidhi vifaa hivyo amesema kwa Ikungi wana oda ya kupeleka vifaa vya Shilingi Milioni 300 na kuishukuru serikali kwa kuwaamini.

"Tumeendelea kuleta vifaa na hivi karibuni tutaleta vifaa vilivyobakia ikiwemo mashine ya usingizi wakati wa kufanya upasuaji kwa wagonjwa,"amesema.

Diwani wa Kata ya Unyahati Abbely Surry amempongeza sana mbunge kwa kuendelea kuwa sauti ya wananchi bungeni kwa kuwa hayo ni matokeo ya uwakilishi wake mzuri.

"Sasa wananchi wanapata huduma jirani tofauti na awali na wananchi wenye kipato kidogo ilikuwa changamoto kupata huduma,lakini kwa sasa imekuwa nafuu kwao,"amesema.

Mganga Mkuu Wa Wilaya ya Ikungi Dr Dorisila John ameeleza ujio wa vifaa hivyo kiwa utawezesha upatikanaji wa huduma zilizokuwa hazijaanza kutolewa ziweze kutolewa kwa wananchi.

"Mbali na vifaa hivi tunaishukuru serikali kwa kuwa wameshaleta na waganga wa kutosha kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa aina zote,".amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com