Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHE. KATAMBI: RAIS SAMIA ANAWAJALI WATU WENYE ULEMAVU

 

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema ofisi hiyo imeanza mchakato wa mapitio ya Sera ya Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 2004 ili kukidhi mahitaji ya sasa.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo mahsusi ya Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan na maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mhe. Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko.

Akizungumza Novemba 23, 2023 aliposhiriki kipindi cha Malumbano ya Hoja kinachorushwa na ITV, kwa njia ya simu kilichofanyika jijini Mwanza, Mhe. Katambi amesema Rais Samia anawajali Watu wenye Ulemavu na ndio maana ameelekeza kufanyika kwa mapitio hayo ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi, kijamii, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, stahiki na afua zinazostahili wenye Ulemavu.

“Tumeanza mchakato na wadau tutawashirikisha hatua kwa hatua katika mapitio ya sera hii na itasaidia kutunga sheria au kufanya mabadiliko ya Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2010 ili iendane na mahitaji ya sasa, tukumbuke ndugu zangu hojafa hujaumbika haya mambo lazima tuyafanye kwa uchungu mkubwa, serikali na wadau wa maendeleo ni jukumu letu sisi kuwahudumia wenye ulemavu,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com