MWILI WA SALU NDONGO WAAGWA SHINYANGA, KUZIKWA SIMIYU

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ameongoza Wananchi na Watumishi wa Serikali Manispaa ya Shinyanga, katika Maombolezo ya kuuaga mwili wa marehemu Salu Ndongo ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji Manispaa ya Shinyanga, Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini.

Marehemu Ndongo alikuwa Mtumishi wa Serikali Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, alifariki dunia Novemba 17 eneo la Barabara ya Kalogo Mjini Shinyanga kwa ajali ya gari yake, na mwili wake umeagwa leo katika Kanisa la Wasabato Shinyanga, na umesafirishwa leo hii kwenda nyumbani kwake Jijini Mwanza, ambapo kesho atasafirishwa kwenda kuzikwa kwao katika kijiji cha Gangabilili wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza wakati wa kutoa salamu za Rambi Rambi, amesema aliupokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa, huku akiwasihi wanadamu kila mmoja anapaswa kujiweka tayari sababu hakuna anaye jua siku wala saa ya kufikwa na umauti.

Amesema Serikali inatoa pole kwa watumishi wote, pamoja na familia ya wafiwa, huku akimpatia neno la faraja mjane wa marehemu, kwamba ashike sana msalaba na kumtumainia Yesu sababu yeye ndiyo mfariji na ni Baba wa Yatima na Wajane.
Nao baadi ya viongozi mbalimbali wakitoa salama za Rambi Rambi akiwamo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Elias Masumbuko na Ofisi ya Mbunge Katambi, wametoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu huku wakieleza kuwa msiba huo ni pigo kubwa.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini Razalo Mbogo, amesema msiba huo umegusa watu wengi sababu marehemu ndongo alikuwa akigusa maisha ya watu kutokana na utendaji wake kazi katika idara hiyo ya Ardhi.
RC Mndeme (kushoto) akimpa pole Mjane.

“Marehemu Salu Ndongo nimemfahamu kwa muda mfupi sana, alikuwa mtu mwenye kuangalia watu na kuhudumia haraka, hata mimi ameshawahi kunipatia huduma, nilipopata taarifa za msiba wake nilishutuka sana,”amesema Mchungaji Mbogo.

“Mungu anaponyamaza kimya kwa jambo lolote subiri na Mshukuru na usifadhaike Moyoni mwako, kifo cha Salu Ndongo huwezi jua kwanini Mungu alinyamaza, Mjane unapoona Mbingu zimenyamaza mtegemee Mungu, Yohana 14 inasema msifadhaike mioyoni mwenu mnamwanini Mungu niaminini na mimi,”ameongeza Mchungaji Mbogo.
Aidha, amesema kupitia Msiba huo uwasogeze watu kuwa karibu na Mungu na kumtanguliza kwa kila jambo pamoja na kuhudhuria Ibada Kanisani, siyo mtu akipatwa na Matatizo ndipo anamkumbuka Mungu, na kubainisha kwamba maandiko yanasema katika Kitabu cha Zaburi 90 kuwa siku za Mwanadamu kuishi ni miaka 70 akiwa na nguvu miaka 80.

Mtoto wa Marehemu Deogratius Ndongo akisoma Wosia wa Marehemu Baba yake, amesema alizaliwa mwaka 1967 katika Kijiji cha Gangabilili wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, na amefariki akiwa na miaka 56 ameacha Mjane na watoto Watatu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa salamu za rambirambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo katika Kanisa la Wasabato Shinyanga Mjini kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Jijini Mwanza kisha nyumbani kwao Kijiji cha Gangabilili wilaya ya Itilima mkoani Simiyu kwa ajili ya mazishi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akitoa salamu za Rambi Rambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mchungaji wa Kanisa la Wasabato Shinyanga Mjini Razalo Mbogo akiongoza Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akitoa salam za Rambi Rambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akitoa salamu za Rambi Rambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akitoa salamu za Rambi Rambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mwenyekiti wa Wazazi CCM akitoa salamu za Rambi Rambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Nassoro Warioba akitoa salamu za Rambi Rambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akitoa salamu za Rambi Rambi kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mtoto wa Marehemu Salu Ndongo akisoma Wosia wa Baba yake.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa na viongozi wengine kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akimpa pole na faraja Mke wa Marehemu Salu Ndongo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akimpa pole na faraja Mke wa Marehemu Salu Ndongo.
Viongozi wa Kanisa la Wasabato wakiwa kwenye Ibada ya kumuombea na kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa na viongozi wengine kwenye Ibada ya kumuaga Marehemu Salu Ndongo.
Ibada ya kumuombea na kumuaga Marehemu Salu Ndongo ikiendelea.
Ibada ya kumuombea na kumuaga Marehemu Salu Ndongo ikiendelea.
Ibada ya kumuombea na kumuaga Marehemu Salu Ndongo ikiendelea.
Ibada ya kumuombea na kumuaga Marehemu Salu Ndongo ikiendelea.
Mwili wa Marehemu Salu Ndongo ukiwa katika Sanduku.
Familia ya Marehemu Salu Ndongo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Salu Ndongo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Salu Ndongo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa na viongozi mbalimbali wakiaga mwili wa Marehemu Salu Ndongo.
Zoezi la kuaga mwili wa Marehemu Salu Ndongo likiendelea.

Familia ya Marehemu Salu Ndongo wakiuaga Mwili wa mpendwa wao.
Familia ya Marehemu Salu Ndongo.
Mwili wa Marehemu Salu Ndongo ukiwa umebebwa kwa ajili ya kupakiwa kwenye gari kwenda nyumbani kwake Mwanza ambapo kesho utapelekwa Simiyu kwa mazishi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post