NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UN Women duniani na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Dkt.Phumuzile Mlambo Ngeuka amewasili nchini leo Novemba 6,2023 usiku huu kwaajili ya kushiriki katika Tamasha la 15 la Jinsia ambalo linatarajiwwa kufanyika Novemba 7-10, 2023 katika Viwanja vya TGNP, Mabibo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi TGNP Mtandao, Bi.Gemma Akilimali na Mkurugenzi wa TGNP, Bi.Lilian Liundi walikuwa na jukumu la kumpokea mgeni huyo ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha hiloKatika Tamasha hilo takribani watu zaidi ya 2000 wanategemewa kushiriki wakiwemo wawakilishi wa asasi za kirai kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi mbalimbali na wananchi kwa ujumla.
Vilevile wageni kutoka nchi 14 kutoka mabara matatu duniani watashiriki, nchi hizo ni Ghana, Canada, Korea Kusini, India, Haiti, Eswatini, Afrika Kusini, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe, Bangladesh, Uganda, Kenya na Tanzania.
Social Plugin