Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DUWASA YAENDELEZA UIMARISHAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI

 


Na Mwandishi Wetu,Dodoma

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa  mazingira Dodoma (DUWASA) imeendelea kufanya matengenezo ya mabomba yaliyopasuka yanayosambaza huduma ya maji katika makazi ya wananchi ili kurejesha na kuimarisha huduma ya majisafi. 

Leo Novemba 30,2023, Idara ya Ufundi ikishirikiana na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma - DUWASA wameendesha zoezi maalum la kuyafikia maeneo yenye changamoto ya kupasuka mabomba na kuvujisha maji katika maeneo ya Nzuguni na Njendengwa Mashariki katika kuhakikisha yanawekwa mabomba mapya na vifaa vipya ili huduma ya upatikanaji wa majisafi kwa wananchi irejee kwa uhakika. 

Wananchi wa Mtaa wa Machaka, Kata ya Nzuguni wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikishia majisafi majumbani na kuishukuru DUWASA kwa hatua waliyoichukua kwa kufanya kutekeleza mradi mkubwa wa maji. 

Edwin James Nassoro ni Fundi wa Kanda namba 3 na 4 Nzuguni, ambaye amesema eneo la Nzuguni linaathirika mara kwa mara kwa mabomba ya maji kupasuka kutokana na msukumo mkubwa wa maji ambayo kwa sasa yameanza kupatikana baada ya mradi mkubwa wa maji wa Nzuguni kuanza kutoa huduma kwa wananchi katika baadhi ya maeneo hayo. 

DUWASA imenuia kuhakikisha kufika kila eneo inalohudumia kutatua changamoto za uhaba wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com