Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Timu ya Wanawake JKT Queens ambayo inatarajia kutupa karata zake za kwanza dhidi ya Mamelodi Sundowns Ladies katika Mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa Wanawake Barani Afrika Mchezo utakaopigwa kesho Novemba 5, 2023 Jijini Abdijan nchini Ivory coast.
Na.Alex Sonna-DODOMA
TIMU ya Wanawake ya JKT Queens imekamilisha Maandalizi ya Mwisho Kuwakabili Mamelodi Sundowns Ladies katika Mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa wanawake Barani Afrika Mchezo utakaopigwa kesho Novemba 5, 2023 Jijini Abdijan nchini Ivory coast.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 4,2023 jijini Dodoma Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema kuwa wamekamilisha maandalizi ya mchezo huo na wachezaji wapo tayari kuibuka na ushindi siku ya kesho.
Brigedia Jeneral Mabena amesema kutokana na kuwa na wachezaji wengi wanaocheza timu ya taifa ya wanawake Twiga Star itakuwa chachu ya wao kufanya vizuri kwenye Michuano hiyo.
''Mikakati ya JKT ni kufanya vizuri na kuchukua Kombe hilo uwezo wa kufanya hivyo tunao kutokana na kuwa na kikosi bora chenye kuleta ushindani katika mashindano yoyote kwani tuna benchi la ufundi lenye uwezo wa kuyatimiza malengo waliyojiwekea kama Taasisi.''amesema Brigedia Jeneral Mabena
Amesema JKT Queens jana imefanya mazoezi majira ya saa moja usiku katika uwanja wa lycee moderne uliopo mji wa korhogo Ivory coast ikiwa ni maandalizi ya mchezo wake huo wa kesho.
Brigedia Jeneral Mabena amesema timu hiyo imejipanga vyema na kwamba inawahakikishia watanzania kuwa wanakwenda kupata matokeo mazuri.
Timu ya JKT Queens inashiriki Michuano hiyo baada ya bingwa wa CECAFA kwa kuifunga C.B.E ya Ethiopia kwa Mikwaju ya Penalti 5-4 baada ya dakika 90 kuisha kwa sare ya bila kufungana.
Hii inakuwa mara ya pili timu kutoka Tanzania kushiriki Michuano hiyo baada ya msimu uliopita Simba Queens Kuchukua Ubingwa wa CECAFA na kuishia nusu Fainali ya CAF.
Baada ya Mchezo wa Kesho JKT Queens watacheza na weneji Atlentico Abidjan ya Ivory Coast Novemba 8 ,majira ya saa mbili usiku na kumaliza na Casablanca ya Morocco Novemba 11,JKT imepangwa kundi A.
Social Plugin