Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHAFALI YA 15 KOM SEKONDARI YAFANYIKA.... RPC MAGOMI AIMWAGIA SIFA INAVYOUTANGAZA VIZURI MKOA WA SHINYANGA

Na Amos John Shinyanga

Mahafali ya 15 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Jumamosi Novemba 25,2023 ambapo jumla ya wanafunzi 142 wamehitimu elimu ya kidato cha nne mwaka 2023.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo yaliyohudhuriwa na wazazi na wageni mbalimbali mgeni rasmi, Kamanda wa Polisi mkoa Wa Shinyanga ACP Janeth Magomi ameipongeza shule ya Sekondari Kom kwa kuendelea kufanya vizuri kitaaluma hali inayoutangaza mkoa wa Shinyanga.

"Mabadiliko yoyote yanaletwa na ushirikiano hivyo kupitia ushirikiano shule hii imekuwa maarufu nchini kutokana na elimu bora inayotoa na kutokana na hali hiyo imeupatia sifa mkoa wa Shinyanga. Sisi kama serikali tunajivunia uwepo wa shule hii katika mazingira yetu kwani inatutangaza, tupo tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto zinazojitokeza ili kusukuma gurudumu la maendeleo”,ameeleza Kamanda Magomi.

Aidha ameipongeza shule hiyo kwa malezi bora ya wanafunzi hali inayosaidia kupunguza vitendo vya ukatili mkoani humo huku akitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi kuwekeza kwenye elimu kwa watoto kwani huo ndiyo urithi wenye thamani katika maisha yao.

Magomi amewataka wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kuwa mfano katika maeneo wanakokwenda na kuhakikisha matendo yao yanaendana na mambo waliyofundishwa shuleni.

Katika hatua nyingine Kamanda Magomi ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha shule ya awali na msingi kitendo ambacho kinatokana na ushirikiano uliopo kati ya shule na wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kusukuma maendeleo ya shule.

Naye Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi ameishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapa katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inafikia malengo yake.Amesema Kom sekondari tangu kuanzishwa kwake imekuwa daraja la elimu kwa wanafunzi ambao wengi wamekuwa wakiingia kidato cha tano na kujiunga katika vyuo mbalimbali.

“Naomba wazazi muendelee kutuamini na kuleta wanafunzi katika shule hii ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali”,ameeleza Koyi.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne,Caster Godfrey amesema walianza kidato cha kwanza wakiwa 131, lakini idadi iliongezeka na hivyo idadi ya waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 142.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa Washinyanga ACP Janeth Magomi akimtunuku Cheti mmoja wa wahitimu wa elimu ya kidato cha nne mwaka 2023 katika shule ya Sekondari Kom 
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom Jackton Koyi akimpa mkono wa hongera kaka mkuu wa Shule hiyo
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akipokea risala kutoka kwa mkuu wa shule hiyo.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akimtunuku Cheti mmoja wa wahitimu wa elimu ya kidato cha nne mwaka 2023 katika shule ya Sekondari Kom 

Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi akimkabidhi zawadi mgeni rasimi Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi

Wahitimu wa elimu ya kidato cha nne mwaka 2023 katika shule ya Sekondari Kom wakicheza wakati wa mahafali

Wahitimu wa elimu ya kidato cha nne mwaka 2023 katika shule ya Sekondari Kom wakifurahia wakati wa mahafali

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com